Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Zimbabwe yajiandaa kwa maandamano zaidi

Maandamano makubwa yanatarajiwa jijini Harare, Zimbabwe, kushinikiza kufanyika mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, maandamano ambayo Polisi imesema ni batili.

Viongozi wa upinzani nchini Zimbabwew, Morgan Tsvangirai (kushoto) na Joice Mujuru (kulia) wakiwa kwenye moja ya maandamano
Viongozi wa upinzani nchini Zimbabwew, Morgan Tsvangirai (kushoto) na Joice Mujuru (kulia) wakiwa kwenye moja ya maandamano REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Hapo jana viongozi walioandaa maandamano hayo waliwasilisha shauri katika mahakama kuu wakiomba iwaagize Polisi kuwapa ulinzi maelfu ya waandamanaji watakojitokeza katika kile walichosema ni maandamano ya amani kushinikiza mabadiliko.

Polisi imeonya kufanyika kwa maandamano hayo, ambapo imewataka waandaaji wa maandamano hayo kuwasilisha shauri katika mahakama kuu kuomba madai yao yasikilizwqe kuliko kuandamana.

Ikiwa maandamano haya yatafanyika licha ya oingamizi la Polisi, yanakuja ikiwa ni siku mbili tu zimeoita toka kushuhudia maandamano mengine ya vijana wa chama cha upinzani waliokabiliana na Polisi mjini Harare wakipinga unyanyasaji unaofanywa na Polisi.

Kwa miezi kadhaa hivi sasa nchi yas Zimbabwe imeshuhudia maandamano makubwa kushinikiza kuondoka madarakani kwa rais Robert Mugabe, pamoja na kupinga hali ngumu ya maisha nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.