Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Shughuli za rejea kama kawaida Harare

Shughuli zimerejea kwenye hali ya kawaida jijini Harare, Zimbabwe baada ya Jumatano ya Agosti 24, kushuhudia maandamano ya vijana wa upinzani waliokuwa wanapinga unyanyasaji unaofanywa na jeshi la Polisi nchini humo.

Mmoja wa waandamanaji nchini Zimbabwe akiwa na bango linaloshinikiza Rais Mugabe aondoke madarakani
Mmoja wa waandamanaji nchini Zimbabwe akiwa na bango linaloshinikiza Rais Mugabe aondoke madarakani REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Polisi kwa mara nyingine walitumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya maelfu ya vijana wa chama kikuu cha upinzani nchini hujmo cha MDC, waliokuwa wakiandamana kwenda wizara ya mambo ya ndani kuwasilisha malalamiko yao.

Vurugu zilitokea baada ya Polisi kuikngilia kati maandamano ya vijana hao, ambao walikuwa na mabango yaliyokuwa yanakashifu nguvu kubwa inayotumiwa na Polisi dhidi ya raia.

Baada ya kuzuiwa na Polisi na kuanza kurushiwa vitoa machozi, waandamanaji waligeuza maandamano yao kuwa uwanja wa vita na kuanza kukabiliana kwa mawe na kikosi cha Polisi wa kutuliza ghasia.

Hata hivyo hali imerejea kuwa ya utulivu siku ya Alhamisi ambapo wananchi wameonekana wakiendelea na shughuli zao za kawaida kwenye viunga vya jiji la Harare na maeneo meninge ya nchi ambakok maandamano kama haya yalikuwa yamepangwa kufanyika.

Polisi nchini Zimbabwe imeonya kuhusu kufanyika kwa maandamano mengine, na kuapa kuwa jeshi hilo halitasita kutumia nguvu kuwatawanya waandamanaji ambao linasema hawakuwa na kibali cha kuandamana.

Jeshi la Polisi nchini Zimbabwe hivi karibuni limejikuta kwenye shinikizo kubwa na kukosolewa kwa sehemu kubwa na makundi mbalimbali ya watetezi wa haki za binadamu wanaodai kuwa limekuwa likitumia nguvu kubwa kuwakabili waandamanaji.

Upinzanik nchini humo unakosoa Serikali ya Rais Mugabe, ambaye wanamtuhumu kwa kuiendesha nchik yao kiimla, huku akidharau maoni ya wananchi na wanasiasa kuhusu namna ya kuinusuru nchik hiyo na hali mbaya ya kiuchumi.

Hivi karibuni nchi hiyo ilishuhudia maandamano makubwa kuwahi kutokea, ambayo yaliitishwa na mmoja wa wahubiri maarufu nchinik humo aliyeitisha mgomo wa nchi nzima kushinikiza kuondoka madarakani kwa Rais Robert Mugabe na Serikali yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.