Pata taarifa kuu
CHAD-UCHAGUZI-SIASA

Chad: askari wote waliotoweka bado "hai"

Upinzani nchini Chad unalaani kutoweka kwa askari ambao hawakumpigia kura Rais anaye maliza muda wake Idriss Deby Aprili 9. Mapema wiki hii, kiongozi wa upinzani, Saleh Kebzabo alizungumza kuhusu askari sitini waliotoweka ambapo miili ya baadhi ya askari hao ikiokotwa pembezoni mwa mto.

(Picha ya zamani) Askari wa Chad mbele ya mahakama ya N'djamena.
(Picha ya zamani) Askari wa Chad mbele ya mahakama ya N'djamena. © Thomas SAMSON/Gamma-Rapho via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa upinzani ametoa wito wa kuanzisha uchunguzi huru zoezi la uchaguzi kwa wanajeshi. Jumanne, Aprili 19, mashirika ya haki za binadamu pia yalizungumzia kuhusu kutoweka kwa askari hao, huku yakiomba kufanyika kwa uchunguzi.

Raia wa Chad walipiga kura Aprili 10, ispokua wanajeshi, ambao walipiga kura siku moja kabla, Aprili 9. Tangu wakati huo, hakuna taarifa ya askari sitini miongoni mwa wanajeshi wa taifa, kwa mujibu wa kiongozi wa upinzani, Saleh Kebzabo. Amethibitisha kwamba miili iliookotwa pembezoni mwa mto Chari ilikua na kovu za mateso waliyoyapata askari hao

Viongozi wa kijeshi katika vituo vya kupigia kura?

Mashirika ya haki za binadamu kwa sasa, yamekusanya ushuhuda kutoka familia 21 ambazo hazina taarifa ya ndugu zao. Banadji Pirho, kiongozi wa shirika linaloendeleza Uhuru wa msingi nchini Chad, akiwa piai msemaji wa muungano wa mashirika sita ya haki za binadamu amesema kuwa walipata taarifa kutoka baadhi ya familia kuhusu kuwepo kwa viongozi wa kijeshi katika vituo vya kupigia kura. "Tuliarifiwa na ndugu wa askari waliotoweka, ambao walidai kuwa wakati wa zoezi la uchaguzi la Aprili 9, inaonekana kwamba viongozi wa kijeshi walikua katika vituo vya kupigia kura kuchunguza wale ambao hawakumpigia kura rais anaye maliza muda wake na baadaye walikamatwa na kuteswa, kulingana na ushahidi tuliopokea, " Pyrrhus Banadji amesema.

Pyrrhus Banadji ameomba uchunguzi uanzishwe haraka iwezekanavyo ili kujua ukweli. "Tunaomba askari wanaozuiliwa katika maeneo ya siri waachiliwe huru bila masharti. Tunaomba pia uchunguzi huru uanzishwe ili kuwatambua wahusika na kuwaadhibu kwa mujibu wa sheria kutokana na vitendo vya kinyama na kikatili, " Pyrrhus Banadji ameongeza.

"Madai ya uongo"

Serikali imefutilia mbali madai hayo na kusema kuwa ni "madai ya uongo." Waziri wa Mawasiliano, Mustapha Ali Alifeï amesema kwamba askari wote "waliotoweka" bado "hai" na kwamba mwanga utatolewa "katika siku chache."

Katika vyombo vya habari, Waziri wa Usalama wa Raia, Bashir Ahmad Mahmat, amesema kuwa wanajeshi wanaotumwa kwa mambo ya kazi "hawapaswi kila mara" kufahamisha familia zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.