Pata taarifa kuu
MOROCCO-BAN-UNSC

Ban Ki-moon ataka kurejeshwa kwa ujumbe wa UN Sahara Magharibi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon analitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuishinikiza Morroco kurejesha ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo linalojitegemea la Sahara Magharibi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. © REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Ban ameonya katika ripoti yake kwa wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa ikiwa wajumbe hao watarejelea shughuli zao katika eneo hilo, usalama wao unasalia hatarini.

Serikali ya Morroco iliwafukuza wafanyikazi 83 waliokuwa wanafanya kazi katika eneo la Sahara Magharibi mwezi uliopita na kufunga Ofisi ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa.

Ban Ki-moon ambaye alizuru eneo hilo miezi kadhaa iliyopita, aliishtumu serikali ya Morroco kwa kuendelea kuzuia uhuru wa eneo la Sahara Magharibi.

Onyo hili la Ban Ki-moon linakuja huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kupiga kura wiki ijayo kupitisha azimio la kuendelea kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katka eneo la Sahara Magharibi tangu kuzinduliwa kwake mwaka 1991.

Ujumbe huo wa MINURSO unatarajiwa kuendelea katika eneo hilo hadi Aprili mwaka 2017.

Eneo la Sahara Magharibi limeendelea kuishinikiza dunia kuisaidia kujitenga na kuwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.