Pata taarifa kuu
MOROCO-POLISARIO-UHASAMA

Polisario yaonya hatari ya kuzuka kwa uhasama

Kiongozi wa kundi la Polisario Front, ambaye anadai uhuru wa Sahara Magharibi, ameonya Umoja wa Mataifa Alhamisi hii hatari ya kuanza kwa uhasama na Morocco ikiwa Umoja wa Mataifa nchini humo (MINURSO) hatoweza kuendesha kikamilifu wajibu wake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alikutana na Ahmed Boukhari, mwakilishi wa Polisario katika Umoja wa Mataifa, karibu na kambi ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Bar-Lahlou, kilomita 220 kusini magharibi mwa mji wa Algeria wa Tindouf.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alikutana na Ahmed Boukhari, mwakilishi wa Polisario katika Umoja wa Mataifa, karibu na kambi ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Bar-Lahlou, kilomita 220 kusini magharibi mwa mji wa Algeria wa Tindouf. Farouk Batiche / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa kundi la Polisario Front Mohamed Abdelaziz akisherehekea maadhimisho ya miaka 35 ya tangazo la uhuru wa Sahara Magharibi, Februari 27, 2011.
Katibu Mkuu wa kundi la Polisario Front Mohamed Abdelaziz akisherehekea maadhimisho ya miaka 35 ya tangazo la uhuru wa Sahara Magharibi, Februari 27, 2011. AFP PHOTO / DOMINIQUE FAGET

Kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "haitoishinikiza moja kwa moja" Morocco kwa kuruhusu MINURSO "kuanzisha kazi yake na wajibu wake kwa maandalizi ya kura ya maoni ya kujitegemea, basi bila shaka itakua ni ruhsa kwa uvamizi wa kijeshi wa Morocco dhidi ya wakazi wa Shara ya magharibi" amesema Mohammed Abdelaziz.

"Watu Sahara magharibi watalazimika mara nyingine tena kutetea haki zao kwa njia zote halali, ikiwa ni pamoja na mapambano ya silaha, ambayo yalipitishwa na Umoja wa Mataifa kwa watu wote walio chini ya ukoloni," inasema barua kutoka kwa Bw Abdelaziz iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda huo (MINURSO) ulitumwa mwaka 1991 ili kufuatilia mkataba wa usitishwaji mapigano katika Sahara Magharibi kwa kusubiri kukamilika kwa sheria maalum ya eneo hilo, koloni ya zamani ya Uhispania iliyounganishwa na Morocco mwaka 1975.

Wakati wa ziara yake katika Ukanda huo mapema mwezi Machi, Ban Ki-moon alikemea vikali mwenendo wa Rabat inayolichukulia eneo la Sahara Magharibi kama sehemu yake.

Kwa kujilipiza kisasi, Morocco iliwafukuza baadhi ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa na kufunga ofisi ndogo ya kijeshi ya Umoja huo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hatua hizo zinauzuia kufanya kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.