Pata taarifa kuu
UFARANSA-MOROCCO-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

François Hollande na Mohammed VI wamaliza mfarakano kati ya Rabat na Paris

François Hollande na Mfalme Mohammed IV wamejikubalisha kuboresha maridhiano kati ya Ufaransa na Morocco wakati wa ziara ya siku mbili ya Rais wa Ufaransa katika mji wa Tanger, na hivyo kumaliza mfarakano uliyokuwa kati ya nchi hizi mbili.

(Kutoka kushoto kwenda kulia): Mfalme Mohammed VI wa Morocco, Rais François Hollande na Jamel Debbouze kushiriki wakizungumza wakati wa mapumziko katika mji wa Tanger ,Septemba 20, 2015.
(Kutoka kushoto kwenda kulia): Mfalme Mohammed VI wa Morocco, Rais François Hollande na Jamel Debbouze kushiriki wakizungumza wakati wa mapumziko katika mji wa Tanger ,Septemba 20, 2015. AFP/POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hollande ameondoka Jumapili hii katika mji wa Tanger saa 3:00 usiku (saa za Ufaransa) sawa na 2:00 usiku (saa za kimataifa) baada ya siku mbili akiwa ziarani nchini Morocco ambapo ameimarisha uhusiano pamoja na Mfalme wa Morocco.

Matatizo kati ya nchi hizi mbili " sio tu yamefutika, lakini zaidi yamepitwa na wakati ", Rais Hollande amesema Jumapili hii, mbele ya jamii ya raia wa Ufaransawaliokusanyika katika ubalozi mdogo wa Ufaransa katika mji wa Tanger.

Rais wa Ufaransa pia amehakikisha kuwa amefungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya Ufarasa na Morocco.

Lengo la safari hii katika mji wa Tanger, kunakopatikana bandari kubwa kaskazini mwa Morocco, ilikuwa kudhihirisha kuwa mgogoro wa kidiplomasia ulio dumu karibu mwaka mmoja, ambao ulisababishwa na kuwasilishwa kwa mashitaka ya "mateso" nchini Ufaransa dhidi ya mkuu wa Idara ya ujasusi wa Morocco, Abdellatif hammouchi, ulikua umekwisha. Na kwamba wakati umefika wa kufufua mahusiano makubwa kati ya Ufaransa na Morocco, mshirika mkubwa katika masuala ya usalama, siasa na uchumi.

" Tuna ushirikiano ambao unaendelea na hakuna kinachoweza kubaudilisha ", amesema Rais Hollande, akitoa mfano wa usalama. Kwa sababu, amesema, nchi hizi mbili " zinakabiliwa na changamoto moja" katika kupambana dhidi ya ugaidi, hasa kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.