Pata taarifa kuu
UGANDA-USHIRIKINA-WATOTO

NGO-Uganda: watoto watoweka kutokana na imani za kishirikina

Nchini Uganda, watetezi wa haki za watoto wanabainisha kuongezeka kwa uhalifu wa imani za kishirikina wakati wa kampeni za uchaguzi wa hivi karibuni. Kwa uchache watoto saba walitoweka, na ndugu zao wanahofia kuwa huenda walitekwa nyara na baadaye kukatwa viongo vyao vya miili au kuuawa.

Bango la kampeni ya serikali ya Uganda na mashirika yasio ya kiserikali dhidi kafara ya watoto. "Kafara ya mtoto haileti utajiri, tunalaani jambo hili".
Bango la kampeni ya serikali ya Uganda na mashirika yasio ya kiserikali dhidi kafara ya watoto. "Kafara ya mtoto haileti utajiri, tunalaani jambo hili". © DR
Matangazo ya kibiashara

Familia za watoto hao wanaamini kwamba kupotea kwa huko kunaendana na vitendo vya uchawi au imani za kishirikina zenye lengo la kuleta bahati nzuri, shirika la Kyampisi Childcare Ministries limesema.

Kwa kujiwekea bahati nzuri, baadhi ya watu nchini Uganda wanaamini kuwa kafara ya mnyama ni jambo zuri. Wengine, wanaamini kwamba bahati nzuri, ni bora zaidi kumtoa kafara binadamu. Hii ni aina ya hoja inayomtia mashaka Peter Ssewarkiryanga, mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kyampisi Childcare Ministries, shirika la Kikristo lisilo la kiserikali la mjini Kampala.

Kwa mujibu wa shirika hilo, visa saba vya kupotea kwa watoto vilishuhudiwa, kuanzia mwezi Oktoba hadi mwezi Februari, katika wilaya za Ssembabule, Mukono, Mubende na Buikwe, ambapo gazeti la serikali la New Vision tayari limeutaja mji wa Kampala kama "mji mkuu wa kafara kwa mtoto".

Watoto walitoweka wakati wa kampeni za uchaguzi, kwa mujibu wa Moses Binoga, afisa wa Wizara ya ya Mambo ya ndani, shirika la habari la Uingereza la Reuters, limearifu. Hakuthibitisha, hata hivyo, takwimuiliyotolewa na shirika la kutetea watoto la Kyampisi Childcare Ministries.

Kwa mtazamo wa shirika hilo, kupotea kwa watoto hao hivi karibuni ni kitendo cha waganga wanaowaua watato au kuwakata viungo vyao vya miili kwa niaba ya watu vigogo. Uhalifu huu wa kishirikina umeongezeka kwa kiwango cha juu, kwa mujibu wa Peter Ssewarkiryanga, kutokana na ukuaji mkubwa uchumi wa Uganda na kuongezeka ghafla kwa mali hususan nyumba na kadhalika vinachangia kwa imani hizo a kishirikina, hasa katika mji wa Kampala.

"Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya maendeleo ya kiuchumi na kafara kwa watoto. Hakuna shaka, amesema Peter Ssewarkirynga. Katika mji wa Kampala, matajiri ambao hujenga nyumba, wanatoa kafara kwenye sehemu wanakojenga nyumba, ikiwa ni pamoja kafara za binadamu, kwa matumaini kwamba ujenzi huo utakwenda vizuri."

Ukubwa wa tatizo hili ni vigumu dhibiti. Zaidi ya watoto 700 walitekwa nyara mwaka 2013, kwa mujibu wa polisi ya Uganda, lakini ni vigumu kusema ni wa ngapi miongoni mwa watoto hao waliotumiwa kwa imani za kishirikina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.