Pata taarifa kuu
BUGANDA-BESIGYE-SIASA-USALAMA

Kizzya Besigye chini ya ulinzi mkali

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda wa chama cha FDC Kizza Besigye, Jumapili hii alihudhuria ibada katika Kanisa la Angilikana la All Nakasero jijini Kampala chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi.

Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye.
Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye. © AFP PHOTO / ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Polisi wakiwa wamejihami kwa silaha walimzingira kutoka nyumbani kwake katika mtaa wa Kasangati hadi Kanisani na wakasalia nje ya Kanisa wakiwa wamejihami.

Besigye alionekana mtulivu akiwa amebeba Biblia yake akiwa anaaingia Kanisani.

Kiongozi huyo wa upinzani amekuwa chini ya ulinzi mkali nyumbani kwa kile polisi anasalia hatari kwa usalama wa nchi hiyo.

Kizza Besigye amedai kuwa kura ziliibiwa ili kumpa ushindi rais Yoweri Museveni, madai ambayo yamekanushwa na tume ya uchaguzi nchini humo.

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Uganda wameitaka serikali kumwachilia huru Besigye na kumpa haki zake za kutembea popote atakapo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.