Pata taarifa kuu
UGANDA-UCHAGUZI-SIASA

Uganda: Uchaguzi tayari kukosolewa

Nchini Uganda uchaguzi wa wabunge, lakini hasa uchaguzi wa rais ulifanyika jana, Alhamisi 18 Februari. Uchaguzi ambao ulifanyika katika mazingira ya kutatanisha na tayari umepingwa na baadhi ya waangalizi.

Zoezi la uhesabuji kura mbili ya kituo cha kupigia kura cha mji wa Kampala, baada ya kituo hicho kufungwa, Februari 18, 2016.
Zoezi la uhesabuji kura mbili ya kituo cha kupigia kura cha mji wa Kampala, baada ya kituo hicho kufungwa, Februari 18, 2016. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Mitandao ya kijamii ilikatwa katika muda wa siku nzima. Vituo vya kupiga kura vilitakiwa kufungua saa moja asubuhi saa za Afrika ya Mashiriki lakini wapiga kura wakati mwengine walibidi wasubiri mpaka saa sita mchana au sasa saba. Katika baadhi ya maeneo, uchaguzi utaendelea kwa siku ya leo.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa na, katika baadhi ya maeneo, hadi masaa 6 havijafunguliwa kwa zoezi hili hii ambalo lilihitaji muda wa kutosha, ikiwa ni pamoja na kadi tatu ambao zilitakiwa kuwekwa katika sanduku la kura. Aidha, mfumo mpya wa kupiga kura uliomba majaribio kadhaa kabla ya alama za vidole za mpiga kura zitambuliwe.

muda mrefu ambao ulisababisha mvutano na tuhuma. Lakini pia uliosababisha kuahirishwa kwa uchaguzi katikavituo kadhaa vya kupigia kura. Sehemu ya moja ya Waganda watapaswa kurudi kwenye zoezi hili la uchaguzi Ijumaa hii. Vituo 14 vya kupigia kura katika mji mkuu na 22 katika wilaya ya Wakiso, ambapo hasa ni pamoja na mji wa Entebbe vitaendelea na zoezi hili Ijumaa hii.

Waangalizi wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kingereza Commonwealth waangalizi wameshutumu utaratibu uliopangwa wa kuwasubirisha foleni wapiga kura, na kutaja kama "hakuna sababu ya kujitetea kabisa," hasa katika mji mkuuwa Kampala. wamekosoa utaratibu usiokuwa na uaminifu katika mchakato huo wa uchaguzi.

Makosa tayari yamenyooshewa kidole. Mgombea mwanamke kwenye nafasi ya Diwani, anadai kuwa aliweza kupiga kura lakini hakujikuta kwenye daftari la wapiga kura. Katika kitongoji cha Ggaba, kulionekana kadi za kura ambazo zilikua tayari kuwekwa alama katika neema ya Rais Museveni. Hatimaye, baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa maeneo ambayo yalikumbwa na hali hii ni vyale yenye wafausi wengi kutoka upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.