Pata taarifa kuu
UN-UGANDA-UCHAGUZI

Umoja wa Mataifa watiwa hofu na hali inayojiri Uganda

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya sintofahamu inayoendelea kushuhudiwa nchini Uganda hasa baada ya uchaguzi mkuu wa urais uliomalizika siku mbili zilizopita.

Askari polisi wa Uganda mbele ya mlango wa ofisi ya kiongozi mkuu wa upinzani Kizza Besigye, Kampala, Februari 19, 2016.
Askari polisi wa Uganda mbele ya mlango wa ofisi ya kiongozi mkuu wa upinzani Kizza Besigye, Kampala, Februari 19, 2016. RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake Umoja wa Mataifa umesema namna maafisa wa usalama wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi wanapokabiliana na watu wasiokuwa na silaha ambao msimamo wao unaelekea upande wa chama cha upinzani cha FDC.

Ofisi ya haki za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kutiwa wasiwasi kutokana na kuwepo kwa hali ya vurugu inayotisha baina ya rais waUganda na viongozi wa upinzani akiwemo Dkt Kizza Besigye.

Juma lililopita waziri wa mashauriano ya kigeni wa Marekani John Kerry alizungumza na rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa simu na kumwelezea wasiwasi wake kuhusiana na matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati polisi ilipokuwa ikikabiliana na wafuasi wa upinzani.

Hata hivyo Kerry alizungumzia swala la uhuru wa viongozi wa upinzani kando na kujadili hatua ya serikali kufunga mitandao ya kijamii siku ya uchaguzi.

Kuimeibuka hali ya wasiwasi baada ya mauaji ya watu wawili pamoja na operesheni ya polisi ya kamata kamata ya kiongozi wafuasi wa upinzani akiwemo Dkt Kizza Besigye kiongozi wa chama cha FDC kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya urais.

Kiongozi mkuu wa upinzani Uganda, Kizza Besigye, kiongozi wa chama cha FDC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kampala, Februari 16, 2016.
Kiongozi mkuu wa upinzani Uganda, Kizza Besigye, kiongozi wa chama cha FDC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kampala, Februari 16, 2016. REUTERS/James Akena

Itafahamika kwamba Dkt Kizza Besigye alipinga mapema matokeo ya uchaguzi akibaini kwamba uligubikwa na wizi wa kura na udanganyifu wa hali ya juu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.