Pata taarifa kuu
CAR-UCHAGUZI-SIASA

CAR: uchaguzi wafanyika katika hali ya utulivu

Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamepiga kura Jumatano hii kwa juhudi na utulivu katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais na wabunge, hatua muhimu inayopania kuwaondoa katika kipindi cha miaka mitatu ya machafuko ya kidini ambayo yamesababisha nchi hii maskini kutumbukia katika vita kwa wenyewe kwa wenyewe.

Mtu akitupia kura yake katika kituo cha kupigia kura katika eneo linalokaliwa na Waislamu wengi la PK5 jijini Bangui, Desemba 30, 2015.
Mtu akitupia kura yake katika kituo cha kupigia kura katika eneo linalokaliwa na Waislamu wengi la PK5 jijini Bangui, Desemba 30, 2015. ISSOUF SANOGO/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mjini Bangui, katika vituo vingi vya kupigia kura shughuli zimekua zikiendelea baada ya saa 10:00 alaasiri (sawa na saa 9:00 alaasiri saa za kimataifa ) muda uliopangwa kusitisha uchaguzi.

Katika vituo hivyo, zoezi la upigaji kura limeanza kwa kuchelewa, hasa katika eneo linalokaliwa na wa Waislamu wengi la PK-5, katika shule ya Koudoukou, iliyolengwa na makombora ya tarehe 13 Desemba wakati wa kura ya maoni ya katiba. Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu watano.

Jumatano hii, eneo hilo lilikua chini ya ulinzi mkali wa askari wa kulinda amani na wapiga kura wengi, ambao walikua wakiharakia kupiga kura katika hali ya utulivu.

"Ninapiga kura kwa sababu mimi ni Mzalendo. Kwa kujenga nchi, hospitali na hata shule", ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP mmoja wao, Ousman, mwenye umri wa miaka 27.

Juhudi hii imeshuhudiwa katika mji mkuu, ambapo hakuna matukio ya vurugu yaliyoripotiwa mchana kutwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.