Pata taarifa kuu
CAR-UCHAGUZI-SIASA

CAR: Uchaguzi mkuu kufanyika Jumatano

Raia wa Jamhuri ya Afria ya Kati watapiga kura Jumatano hii katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na wa wabunge na kupelekea nchi hiyo kuondoka katika machafuko ya wenyewe kwa wenyewe yaliochochewa kidini kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Maafisa wa Tume ya Uchaguzi wakiandaavifaa vya kura nyenzo kwenye uwanja wa ndege wa Mpoko kwa kura ya maoni ya 13 Desemba 2015, jijini Bangui.
Maafisa wa Tume ya Uchaguzi wakiandaavifaa vya kura nyenzo kwenye uwanja wa ndege wa Mpoko kwa kura ya maoni ya 13 Desemba 2015, jijini Bangui. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Machafuko hayo yameitumbukiza nchi hiyo masikini duniani katika hali ya sintofahamu.
Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na wabunge uliokua ulipangwa kufanyika Jumapili Desemba 27, ulisogezwa mbele siku tatu. uamzi huo ulichukuliwa kutokana na matatizo ya vifaa, matatizo ambayo yalikua yanahitaji muda wa siku kadhaa kuwa yamepatiwa ufumbuzi.

Uamuzi huo ulichukuliwa na rais Catherine Samba-Panza baada ya mkutano na wawakilishi wa taasisi za mpito na jumuiya ya kimataifa.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mahamat Kamoun, alitangaza Alhamisi kwamba duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika Jumapili uliahirishwa kwa muda wa siku tatu kutokana na matatizo ya vifaa.

Waziri mkuu wa serikali ya mpito alieleza kwamba masanduku ya kura kwa ajili ya uchaguzi ambao utakamilisha mchakato wa mpito wa kidemokrasia nchini humo, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 2013-2014, yalichelewa kuwafikia na kwamba baadhi ya maafisa watakaosimamia uchaguzi bado hawajapatiwa mafunzo ya kutumia masanduku hayo.

"Inabidi kufanya hivyo kwa vifaa vya kisayansi ili kuzuia udanganyifu. Uamzi wa kuahirishwa kwa uchaguzi huo ni muhimu kama tunataka kuwa na matokeo mazuri", alisema Mahamat Kamoun.

Uchaguzi ambao tayari umeahirishwa mara kadhaa, hatimaye utafanyika Jumatano Desemba 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.