Pata taarifa kuu
CAR-UCHAGUZI-SIASA

CAR: uchaguzi waahirishwa hadi Desemba 30

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na wabunge uliokua umepangwa kufanyika Jumapili Desemba 27 nchini Jamhuri ya afrika ya Kati, umesogezwa mbele siku tatu. uamzi huo umechukuliwa kutokana na matatizo ya vifaa, matatizo ambayo yanahitaji muda wa siku kadhaa kuwa yamepatiwa ufumbuzi

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umechukuliwa na rais Catherine Samba-Panza baada ya mkutano na wawakilishi wa taasisi za mpito na jumuiya ya kimataifa.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mahamat Kamoun, ametangaza Alhamisi kwamba duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika Jumapili umeahirishwa kwa muda wa siku tatu kutokana na matatizo ya vifaa.

Waziri mkuu wa serikali ya mpito ameeleza kwamba masanduku ya kura kwa ajili ya uchaguzi ambao utakamilisha mchakato wa mpito wa kidemokrasia nchini humo, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 2013-2014, yalichelewa kuwafikia na kwamba baadhi ya maafisa watakaosimamia uchaguzi bado hawajapatiwa mafunzo ya kutumia masanduku hayo.

"Inabidi kufanya hivyo kwa vifaa vya kisayansi ili kuzuia udanganyifu. Uamzi wa kuahirishwa kwa uchaguzi huo ni muhimu kama tunataka kuwa na matokeo mazuri", amesema Mahamat Kamoun.

Uchaguzi ambao tayari umeahirishwa mara kadhaa, hatimaye utafanyika tarehe 30 Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.