Pata taarifa kuu
MISRI-UCHAGUZI-SIASA

Misri: duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge kuanza

Raia wa Misri wamepiga kura Jumanne hii Oktoba 27 kwa duru ya pili ya uchauzi wa wabunge, bila kuwepo kwa vyama vya upinzani, katika neema ya Rais Abdel Fattah al-Sisi, ambaye alimng'oa madarakani mtangulizi wake, Mohamed Morsi, miaka miwili iliyopita.

Raia huyo wa Misri aweka kura yake katika sanduku la kura katika kituo cha kupigia kura cha mjini Cairo katika duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge Oktoba 27, 2015.
Raia huyo wa Misri aweka kura yake katika sanduku la kura katika kituo cha kupigia kura cha mjini Cairo katika duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge Oktoba 27, 2015. KHALED DESOUKI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura wachache walikua wameitikia zoezi hilo katika vituo vya kupigia kura katika masaa ya mwanzo, kama walivyoarifu waandishi wa shirika la habari la Ufaransa la AFP waliotembelea vituo hivyo katikati mwa mji wa Cairo.

Duru ya kwanza ya uchaguzi huo tata na orodha inayochukua muda wa wiki sita sasa, havikua na shauku Oktoba 18 na 19 katika nusu ya majimbo 27 ya nchi: 26.5 % tu ya wapiga kura waliosajiliwa walipiga kura.

Waziri Mkuu Ismail Sharif Jumanne wiki hii ametoa witokwa " raia wote wa Misri kushiriki kwa wingi katika (uchaguzi) huu muhimu kwa kuchagua wawakilishi wao", akisisitiza kwamba "raia wanatakiwa kuamua kiwango cha ushiriki ".

Nusu nyingine ya majimbo nchini humo watapiga kura katika duru ya pilii kuanzia Novemba 22 na 23 na zoezi hilo litamalizika na duru ya pili ambayo imepangwa kufanyika Desemba 1 na 2.

Baadhi vituo vya kupigia kura ambako wametembelea waandishi wa shirika la habri la Ufaransa la AFP mapema asubuhi jijini Cairo vilikua tupu karibu vyote, kama shule ya msingi katika kata ya Dokki ambapo watu wawili tu walipiga kura saa moja baada ya ufunguzi wa vituo vya kupigia kura . Chini ya wapiga kura 20 walifuata, kwa mujibu wa mmoja wa maafisa wa tume ya uchaguzi.

Wagombea wanne tu walichaguliwa katika duru ya kwanza ya tarehe 18 na 19 Oktoba, wengine wanapambana upya Jumanne na Jumatano katika duru ya pili katika majimbo 14 kwa jumla ya 27. Katika tukio lolote, orodha na wagombea binafsi waliojiandikisha, karibu wote wanaonekana kuiunga mkono serikali ya Abdel Fatah Al Sissi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.