Pata taarifa kuu
UFARANSA-CONGO-KATIBA-SIASA

Ufaransa yabadili msimamo kuhusu kura ya maoni Congo

Katika hali hii ya mvutano kabla ya kura ya maoni nchini Congo-Brazzaville, Ofisi ya rais wa Ufaransa imetoa msimamo wake mpya juu ya hali inayojiri nchini humo.

Rais wa Ufaransa François Hollande katika Ikulu ya Elysée.
Rais wa Ufaransa François Hollande katika Ikulu ya Elysée. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Katika ndogo ya Ikulu ya Elysée iliyotumwa kwenye vyombo vya habari, François Hollande amesema " anaunga mkono uhuru wa kujieleza " nchini Congo-Brazzaville na amekumbusha kwamba alikuwa ametaka, wakati wa hotuba yake mjini Dakar mwezi Novemba mwaka 2014, kwamba " Katiba zinapaswa kuheshimiwa ".

François Hollande amejaribu kujiweka mbali na Denis Sassou-Nguesso. Wakati wa mkutano wa nchi zinazozungumza Kifaransa mjini Dakar, Novemba 27, 2014, Rais Hollande alionya kwenye RFI kuhusu marais ambao wanataka kubadili sheria kwa kutafuta awamu ya tatu. Hasa, akimaanisha sheria ya kuweka kikomo kwenye umri, akimlenga Rais wa Congo-Brazzaville Denis Sassou-Nguesso.

Julai 7, François Hollande alimpoeka katika Ikulu ya Elysée Rais Denis Sassou-Nguesso kufuatia baada ya rais huyo kumba kukutana kwa mazungumzo na Rais wa Ufaransa. Na katikafursa hilo, wawili hao walikubaliana, katika taarifa yao, kuhusu uwezekano wa kuitisha kura ya maoni ya katiba kwa misingi ya "makubaliano". Jambo ambalo halikutekelezwa nchini Congo-Brazzaville.

Kabla ya Jumatano iliyopita, baada ya kusema kwamba Denis Sassou-Nguesso anaweza kushauriana na watu wake kuhusu kuitishwa kwa kura ya maoni ya Katiba, François Hollande aliwashangaza watu wengi hasa waangalizi ambao wameua wakikosoa msimamo wa Denis Sassou-Nguesso. Jambo ambalo lillisababisha hisisa mbalimbali kuanzi kwa upinzani wa Congo-Brazzaville hadi nchini Ufaransa.

Msimamo wakosolewa

Ijumaa asubuhi wiki hii, chama cha National Front, kupitia sauti ya Louis Aliot, kimeomba serikali ya Ufaransa kujieleza kuhusu msaada wake kwa viongozi wa ya Congo-Brazzaville. Louis Aliot pia ameshutumu hatari ya mabadiliko ya katiba bila ya kuwepo maelewano nchini Congo-Brazzaville. Somo la demokrasia lililotolewa na chama cha National Front kwa Francois Hollande kutoka chama cha Kisoshalisti, si la kawaida.

Leo Ijumaa saa sita mchana, Ofisi ya rais hatimaye imetoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo Rais wa Ufaransa " amelaani vurugu za aina yoyote, ameunga mkono uhuru wa kujieleza na amekumbusha kwamba aliwataka wakati wa hotuba yake mjini Dakar Novemba 29, 2014, viongozi hususan marais kuheshimu Katiba za nchi zao ". Siku mbili baada ya mkutano wake na vyombo vya habari katiak Ikulu ya Elysée, François Hollande anajaribu kujiweka mbali na rais wa Congo-Brazzaville. Kwa sasa Rais Hollande anajaribu kuweka wazi msimamo wa Ufaransa kwa marais kama Denis Sassou-Nguesso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.