Pata taarifa kuu
CONGO-SASSOU-KURA YA MAONI-SIASA

Maandamano kugeuka makabiliano Brazzaville

Mji wa Brazzaville, nchini Congo umeshuhudia Jumanne Oktoba makabiliano makali kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji wanaopinga kura ya maoni ya Katiba inayotazamiwa kufanyika Jumapili mwishoni mwa juma hili.

Vizuizi vyawekwa wakati wa maandamano ya Jumanne, Oktoba 20, mjini Brazzaville.
Vizuizi vyawekwa wakati wa maandamano ya Jumanne, Oktoba 20, mjini Brazzaville. RFI/BH
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano pia yameshuhudiwa katika miji mingine ya nchi hiyo. Watu 4 wameuawa katika makabiliano hayo, ikiwa ni pamoja na watatu jijini Brazzaville, kulingana na idadi ya muda iliyotolewa na serikali.

Mmoja wa viongozi wa upinzani ametolea wito wafuasi wao kuandamana kwa amani, wakati ambapo Waziri wa mambo ya ndani amelaani kuwa ni “uasi ulioandaliwa kwa utaratibu fulani”.

Katika siku sita za kura ya maoni iliyopangwa Jumapili ijayo, wapinzani wa wameendelea kupinga uwezekano wowote wa kufanyika kwa zoezi hilo .

Jumanne usiku wiki hii, Tsaty Pascal Mabiala, Katibu Mkuu wa chama cha UPADS, chama cha kwanza cha upinzani nchini Congo, kimeitisha kwa mara nyingine tena "maandamano ya amani" ili kuzuia kufanyika kwa kura ya maoni ambayo washirika wake wameitaja kuwa ni "mapinduzi ya kikatiba".

Wapinzani wa kura ya maoni walikuwa wametoa onyo hadi Jumatatu jioni kwa Rais Denis Sassou-Nguesso kuwa ameifuta kura ya maoni ya Oktoba 25, na kuahidi kwamba muda huo utakapo tamatika, hawatotambua uhalali wa rais wa Congo.

Angalau watu 4 wameuawa, kwa mujibu wa viongozi

Hatimaye, kuhusiana na mji wa Brazzaville, maandamano dhidi ya kura ya maoni yaligeuka haraka makabiliano na polisi. Siku Jumanne kulishuhudiwa hali ya taharuki katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville. Kwa uchache watu wawili waliuawa kwa risasi, kwa mujibu wa vyanzo vya hospitali na watu wengi walijeruhiwa.

Hata hivyo Jumanne jioni Waziri wa mambo ya ndani, Raymond Mboulou amelaani maandamano hayo ambayo aliyaita kuwa “uasi uliopangwa kwa utaratibu fulani”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.