Pata taarifa kuu
CONGO-SASSOU-KURA YA MAONI-SIASA

Rais wa Congo aitisha kura ya maoni

Kura ya maoni nchini Congo kuhusu ya marekebisho ya katiba itafanyika tarehe 25 Oktoba mwaka huu. Uamuzi huu umetangaza Jumatatu wiki hii baada ya kikako cha Baraza la Mawaziri chini ya uenyekiti wa Rais Denis Sassou Nguesso.

Katika kituo cha kupigia kura cha Brazzaville, Julai 15, 2012.
Katika kituo cha kupigia kura cha Brazzaville, Julai 15, 2012. Photo AFP / Guy-Gervais Kitina
Matangazo ya kibiashara

Nakala ya Katiba mpya ambayo itapendekezwa kwa kura ya raia wa Congo ilikuwa bado haijakamilika Jumanne wiki hii.

Lakini mradi unarejelea kwa kiasi kikubwamapendekezo ya mazungumzo yaliyofanyika katika mji wa Sibiti mwezi Julai, na kikao cha Baraza la Mawaziri kimerejelea mabadiliko makubwa yaliyotajwa.

Nakala hiyo tayari imeanza kupingwa na upinzani, ambao unaona ni mfumo wa "mapinduzi ya kikatiba".

Katika Ibara ya 1 ya mswada wa Katiba (ambayo ina sehemu 241, ziliyogawanywa katika vipengele 21), nchi ya Congo inaelezwa kama madaraka yake yamegawanywa. Ujuzi katika sekta kama vile afya, mipango miji, kilimo, elimu hadi sekondari utawekwa katika serikali za mitaa. Kufutwa hukumu ya kifo na usawa kati ya wanaume na wanawake vitaorodheshwa katika nakala ya msingi. Katika suala la siasa, kanuni ya uhuru katika kujiunga na chama chochote itapewa kipaumbele, sheria kuhusu vyama vya upinzani zitawekwa.

Mabadiliko muhimu zaidi yanahusiana na serikali, na kuundwa kwa wadhifa wa Waziri mkuu ambaye atateuliwa na rais. waziri mkuu, atateuliwa kwa uchaguzi wa mawaziri walioteuliwa na rais. Waziri mkuu atachukua uamzi, kwa kushauriana na rais, kuhusu sera za kiuchumi na kijamii za nchi ambazo ziko ziko chini ya mamlaka yake na serikali yake. Serikali itakua chini ya uangalizi wa Bunge, ambalo limepewa majukumu ya naweza kuifuta serikali kama haitowajibika kwa kazi yake, wakati ambapo rais amepwea uamzi wa kulifuta Baraza la wawakili.

Muhula wa tatu

Muhula wa rais umepunguzwa kutoka miaka 7 hadi 5, lakini rais ana uwezo wa kugombea mara mbili. Umri wa chini kwa wagombea kwa kiti cha urais umepunguzwa hadi miaka 30, kinyume na umri wa miaka 70 uliyowekwa awali. Masharti ambayo yangeweza kumruhusu Rais Sassou Nguesso, mwenye umri wa miaka 72, kugombea awamu ya tatu. Jambo ambalo upinzani unashutumu kuwa ni "mapinduzi ya kikatiba", wakati serikali, inasisitiza kuwa mfumo huo wa maendeleo kwa nchi uzingatiwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.