Pata taarifa kuu
CONGO-KATIBA-SIASA

PCT yajadili kuhusu marekebisho ya Katiba

Kamati Kuu ya chama tawala cha PCT nchini Congo, imekutana jana Jumanne Desemba 30 kwa muda wa zaidi ya masaa 5.

Marekebisho ya katiba yanaweza kumpa nafasi rais Sassou-Nguesso (Picha hapa akiwa mjini Addis Ababa mwezi Januari 2014) kugombea muhula watatu katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka 2016.
Marekebisho ya katiba yanaweza kumpa nafasi rais Sassou-Nguesso (Picha hapa akiwa mjini Addis Ababa mwezi Januari 2014) kugombea muhula watatu katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka 2016. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Lengo la mkutano huo ilikua kujadili kuhusu uwezekano wa kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo ili kumpa nafasi rais wa sasa, Denis Sassou-Nguesso aweze kugombea kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais utakao fanyika mwaka 2016

Ingawa hakuna taarifa rasmi liyotolewa baada ya mkutano, taarifa kutoka kwa baadhi ya walioshiriki mkutano huo zinabaini kwamba wengi wa wa viongozi katika ngazi za juu za chama wamepitisha pendekezo la kuifanyia marekebisho Katiba.

Mkutano huo ulioanza saa mbili usiku (saa za Congo), umemalizika saa nane usiku (saa za Congo). Hata hivyo, msimamo wa wajumbe walioshiriki mkutano huo umeanza kuonekana.

Kwa mujibu wa chanzo kiliyoshiriki katika mijadala mbali mbali ya mkutano huo, kwa jumla ya wajumbe 46 walioshiriki mkutano wameafikiana kuifanyia marekebisho Katiba ya Congo, iliyopitishwa tangu miezi kumi nambili iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.