Pata taarifa kuu
CONGO-SASSOU-KURA YA MAONI-SIASA

Rais wa Congo apania kuitisha kura ya maoni

Rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso ametangaza kuwa kutafanyika kura ya maoni kubaidlisha Katiba ya nchi hiyo.

Rais wa Congo, Denis Sassou-Nguesso.
Rais wa Congo, Denis Sassou-Nguesso. AFP PHOTO / THIERRY CHARLIER
Matangazo ya kibiashara

Ngueso ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 31 sasa amesema tume ya kushughulikia marekebisho ya katiba itateuliwa na kupendekeza marekebisho yanayohitajika kabla ya tarehe ya kura hiyo ya maoni kutangazwa rasmi.

Hii inaamanisha kuwa ikiwa kura hiyo itafanyika, rais huyo mwenye umri wa miaka 71 huenda akawania tena urais kwa muhula mwingine mwaka ujao.

Katiba ya sasa hamruhusu rais Denis Sassou Nguesso kuwania tena urais na wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakipinga kubadilishwa kwa katiba kumpa nafasi nyngine ya kuongoza taifa hilo la Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.