Pata taarifa kuu
KENYA-MGOMO-ELIMU

Kenya: shule zafungua milango baada ya mgomo wa wiki tano 5

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini Kenya wanarudi tena shuleni leo Jumatatu baada ya walimu kusitisha mgomo wao wa wiki tano.

Mji mkuu wa Kenya, ambako mgomo wa waalimu ulishuhudiwa kwa kiasi kikubwa.
Mji mkuu wa Kenya, ambako mgomo wa waalimu ulishuhudiwa kwa kiasi kikubwa. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya walimu nchini humo vinasema vimesitisha mgomo huo baada ya Mahakama kuwataka kufanya hivyo ili kuruhusu mazungumzo kufanyika kwa siku tisini.

Walimu wanadai nyongeza ya mshahara wa kati ya asilimia 50 na 60 na kesi ya nyongeza hiyo inaendelea katika Mahakama ya rufaa.

Wiki iliyopita mgomo wa walimu uliendelea, huku shule nyingi zikifungwa licha ya amri ya mahakama ya kuwataka walimu warejee shuleni Jumatatu.

Wiki iliyopita vyama vya walimu viliripoti mahakamani kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu uamuzi wa Mahakama wa kuwataka walimu kurejea shuleni.
Walimu walijitokeza kwa wingi wakiandamana na viongozi wao wa vyama vya walimu walipojielekeza mahakamani.

Walimu walikwenda mahakamani kutafuta ufafanuzi kuhusu ratiba ya mihula ambayo serikali ilibadilisha mgomo uliposhika kasi.

Wiki mbili zilizopita Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alilihutubia taifa, akisema kinagaubaga kuwa serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.

Rais Kenyatta alitolea wito wadau wote wa elimu nchini Kenya kuketi kwenye meza ya mazungumzo kwa faida ya taifa na wanafunzi ili kuweza kutafutia suluhu mgogoro huo, ambao ametaka utatuliwe kwa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.