Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-SHERIA

Sababu za marufuku ya kurudi kwa Moussa Dadis Camara nchini Guinea

Rais wa zamani wa Guinea aliyefanya mapinduzi ya kijeshi, Moussa Dadis Camara alizuiliwa Jumatano wiki hii jana kuzuiwa kusafiri kwenda Guinea.

Rais wa zamani wa Guinea aliyefanya mapinduzi ya kijeshi, Moussa Dadis Camara, mwaka 2010 Ouagadougou.
Rais wa zamani wa Guinea aliyefanya mapinduzi ya kijeshi, Moussa Dadis Camara, mwaka 2010 Ouagadougou. AFP PHOTO / AHMED OUABA
Matangazo ya kibiashara

Ndege ya Moussa Dadis Camara, ambaye anaishi uhamishoni nchini Burkina Faso tangu mwaka 2010, iliondoka Ouagadougou na ingelitua hatua yake ya kwanza katika mji wa Abidjan kabla ya kuendelea hadi Guinea. Lakini viongozi wa Côte d’Ivoire walimzuia Moussa Dadis Camara kuendelea na safari yake, na ndege ilirudishwa hadi nchini Ghana, kabla ya kurejea Ouagadougou.

Tangu miezi ya hivi karibuni Moussa Camara Daddis alikua akijaribu kurudi nyumbani kwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa rais wa Oktoba 11. rais huyo wa zamani wa Guinea aliyefanya mapinduzi ya kijeshi tayari aliwashangaza wengi kwa kujiunga na cahama cha UFDG cha Cellou Dalein Diallo, mpinzani mkuu wa rais anayemaliza muda wake.

Katika hali hii, haionekani jinsi gani Rais Alpha Condé anaweza kukubali kumpa madaraka Moussa Daddis Camara wakati ambapo anakabiliwa na makosa ya njama za mauaji, utekaji nyara, ubakaji, kuchochea mauaji ya Septemba 28, 2009.
Lakini Moussa Dadis Camara anaonekana kuwa ni mtu asiyekuwa nahofu ya vyombo vya sheria vya Guinea. Anajua kwamba hakuna mwendesha mashitaka ambaye anaweza kumuweka jela kwa kuhofia kuzuka kwa machafuko nchini. Daddis Camara, ambaye ana uhusiano imara ndani ya jeshi bado ni maarufu kwa watu wake, watu wa msituni, kama wanavyoitwa. Kwa mujibu wa chama chake, alitaka " kufika mbele ya vyombo vya sheria, na aweze kuwasilisha faili yake ya ugombea katika uchaguzi wa urais ", ambapo tarehe ya mwisho ni Septemba 1.

Mashitaka kwa "kuhatarisha maisha ya wengine"

Lakini jaribio hili liliorejeshwa nyuma halitobaki bila majibu, kwa mujibu wa mwanasheria wake, Jean-Baptiste Jocamey, ambaye alikuwa pia miongoni mwa watu walikua wakiambatana na Moussa dadis Camara katika safari hiyo. Camara atafungua mashitaka dhidi ya Cote d'Ivoire na Guinea, kwa " kuhatarisha maisha ya wengine ".

" Tulikuwa na dakika 5 ili ndege iweze kutua, wakati mamlaka viongozi wa Côte d’Ivoire walimtaka rubani wa ndege kutotua ndege kataika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Felix Houphouët Boigny ", anasema mwanasheria wa Dadis Camara. Hali ya hatari ambayo itampelekea mteja wake kufungua mashitaka, ameongeza mwanasheria huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.