Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-SHERIA

Dadis Camara ashtakiwa katika kesi ya mauaji ya Septemba 28

Mkuu wa zamani wa kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Guinea, Kapteni Moussa Dadis Camara, ameshtakiwa na mahakama Jumatano, Julai 8 mjini Ouagadougou, kwa kosa la mauaji yaliyotokea Septemba 28 mwaka 2009.

Moussa Dadis Camara alihojiwa na majaji wawili na mwendesha mashtaka kutoka Guinea mjini Ouagadougou kwa zaidi ya masaa mawili, Jumatano Julai 7.
Moussa Dadis Camara alihojiwa na majaji wawili na mwendesha mashtaka kutoka Guinea mjini Ouagadougou kwa zaidi ya masaa mawili, Jumatano Julai 7. AFP PHOTO / AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imethibitishwa na mwanasheria wake, pamoja na wafuasi wa chama chake. Hati hii ya mashtaka inafuatia ziara ziara wiki iliyopita nchini Guinea, ya mwendesha Mahakama mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Fatou Bensouda, ambaye alipongeza " maendeleo muhimu na yenye kuhamasisha " katika uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea nchini Guinea.

Mpaka sasa, Moussa Dadis Camara alikuwa akisikilizwa kwa wakati mmoja kama shahidi katika kesi ya mauaji yaliyotekelezwa katika uwanja wa mpira tarehe 28 Septemba mwaka 2009. Jumatano, Julai 8, Moussa Dadis Camara amehojiwa kwa muda wa masaa mawili na majaji wawili pamoja na mwendesha mashtaka kutoka nchini Guinea kama muhusika katika mauaji hayo.

Tukio hilo lilianza tarehe 28 Septemba mwaka 2009, wakati wa siku kuu ya kitaifa. Vyama vya upinzani vilitoa wito wa kuandamana kwa amani katika uwanja wa mpira mjini Conakry. Lakini wanajeshi na vikosi vya usalama vilivunja maandamano hayo, huku vikiwafanyia mateso ya kikatili waandamanaji. Wakati huo watu 156 waliuawa na wanawake pamoja na wasichana 109 walibakwa.

Mwezi Februari mwaka 2010, vyombo vya sheria vya Guinea vilianzisha uchunguzi wa mauaji. Maofisa kadhaa wa CNDD (Baraza la Taifa la Demokrasia na Maendeleo) walitajwa, ikiwa ni pamoja na Kapteni Moussa Dadis Camara, ambaye wakati huo alikuwa kamanda wa vikosi vya kijeshi. Tume ya kuchunguza mauaji, kula njama za mauaji na ubakaji iliundwa dhidi yake.

Kurejea katika siasa

Moussa Dadis Camara alikanusha mara kadhaa kutokua na hatia. Hati ya mashtaka yake ilipigwa darubini na majengo ya kampeni za uchaguzi mwezi Oktoba. Familia yake inashutumu nia ya kutaka kumuondoa kutoka matarajio yake ya kisiasa.

Cellou Dalein Diallo, kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Guinea (UFDG) ambaye Dadis Camara alitangaza kushirikiana naye atakapo kuwa amerudi nchini, amelani uamzi huo wa vyombo vya sheria nchini Guinea na kusema kwamba Moussa Dadis Camara anafanyiwa madhila hayo kwa sababu za kisiasa. " Nimekua nikipambana dhidi ya tabia ya kutoadhibu wahalifu lakini napinga jinsi vyombo vya sheria vinavyotumiwa kwa malengo ya kisiasa. Na hali hii ndio inayomkuta Dadis camara tangu alipoamua kujiingiza katika siasa, na kuamua kushirikiana na muungano wa vyama vya upinzani (UFDG)", amesema Cellou Diallo Dalein.

Mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini Guinea yamepongeza uamzi huo wa kumfungulia mashtaka mkuu wa zamani wa kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini humo. Mashirika hayo yamesema sheria inapaswa kufuata mkondo wake, na iwapo Moussa Dadis Camara atapatikana na hatia, aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.