Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-SHERIA-HAKI

Wabunge wa Kenya waomba kesi ya Ruto ICC ifutwe

Wabunge wa Kenya wanadai Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuwa inamwonea Naibu rais wa nchi hiyo, William Ruto.

Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto akiwa kwenye mahakama ya ICC kujibu mashtaka ya uhalifu wa kibanadamu inayomkabili
Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto akiwa kwenye mahakama ya ICC kujibu mashtaka ya uhalifu wa kibanadamu inayomkabili Reuters
Matangazo ya kibiashara

Madai haya yanakuja baada ya Majaji katika Mahakama hiyo kukubali ombi la kiongozi wa Mashtaka Fatoue Bensuda kutumia ushahidi wa awali uliorekodiwa wa mashahidi watano ambao walikuwa wamejiondoa katika kesi dhidi ya Ruto kwa madai kuwa walikuwa wamelazimishwa kutoa ushahidi.

Aden Duale kiongozi wa walio wengi bungeni anasema Mahakama hiyo imeendelea kuwa ya kisiasa na kuna njama chafu dhidi ya Ruto.

Ruto anashtakiwa kwa tuhma za kufadhili na kuchochea machafuko baada ya uchaguzi yaliyotokea baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 2007.

Hayo ya kijiri Majaji wa rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, wiki hii waliwaagiza majaji waliokuwa wakisikiliza kesi dhidi ya rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kuamua ikiwa, serikali ya Kenya ilitoa ushirikiano wa kutosha wakati wa kesi ya rais huyo.

Akitoa uamuzi huo, Silvia Fernandez de Gurmend aliwataka Majaji wa Mahakama iliyokuwa ikisikiliza kesi dhidi ya rais Kenyatta kutoa uamuzi sahihi ikiwa serikali ya Kenya ilishirikiana na Mahakama hiyo hasa Ofisi ya kiongozi wa mashtaka wakati kesi dhidi ya rais Kenyatta ilipokuwa inaendelea.

Aidha, Majaji hao wametakiwa kupitia tena uamuzi wao wa kutoiripoti serikali ya Kenya katika Mamlaka iliyounda sheria za Mahakama ya ICC.

Mwaka uliopita, Ofisi ya kiongozi wa Mashtaka iliwataka Majaji waliokuwa wakisikiliza kesi dhidi ya Kenyatta kutoa uamuzi kuwa Naiorbi ilikuwa haitoi ushirikiano kupata ushahidi wa rekodi za kifedha za rais Kenyatta, rekodi ya mazungumzo ya simu na nyaraka zingine muhimu.

Mwaka uliopita kiongozi wa mashtaka Fatoue Bensuda alitanagaza kufuta kesi dhidi ya rais Kenyatta kwa tuhma kuwa serikali ya Kenya ilikuwa imekataa kushirikiana na Ofisi yake na hivyo hakukuwa na ushahidi wa kutosha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.