Pata taarifa kuu
MISRI-JIHADI-MUSLIM BROTHERHOOD

Mwendesha mashtaka wa Misri, Hisham Barakat auawa jijini Cairo

Mwendesha mashtaka wa Serikali ya Misri, Hisham Barakat amefariki dunia akiwa hospitalini, saa chache tu baada ya msafara wake kushambuliwa kwa bomu jijini Cairo, leo Jumatatu.

Baadhi ya viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood ambao hivi karibuni mwendesha mashtaka Hisham Barakat aliiomba mahakama iwahukumu adhabu ya kifo
Baadhi ya viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood ambao hivi karibuni mwendesha mashtaka Hisham Barakat aliiomba mahakama iwahukumu adhabu ya kifo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Akiongea na waandishi wa habari, jijini Cairo, waziri wa sheria, Ahmed al-Zind amethibitisha akiwa hospitalini, kuwa mwendesha mashtaka, Barakat amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.

Tangazo hili linatolewa saa chache tu baada ya kuripotiwa kushambuliwa kwa msafara wa mwendesha mashataka huyo ambapo watu kadhaa waliuawa huku yeye pamoja na maofisa wake wengine wakijeruhiwa kwenye shambulio hili.

Bomu hilo liliharibu majengo kadhaa pamoja na magaro yaliyokuwa jirani kwenye eneo la Heliopolis ambapo kwa mujibu wa polisi magari zaidi ya matano yaliharibiwa vibaya.

Msafara wa Hisham Barakat ulishambuliwa wakati yeye pamoja na walinzi wake walipokuwa wakielekea kwenye makao makuu ya ofisi yake jijini Cairo.

Shambulio hili limetekelezwa saa chache baada ya tangazo la wapiganaji wa kiislamu nchini humo kutangaza vita dhidi ya wafanyakazi wa mahakama hasa majaji ambao wamekuwa wakitoa hukumu kali dhidi ya wafuasi wa kiislamu wa Muslim Brotherhood.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.