Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa rais wa Fifa wafanyika leo

Kufuatia kashfa ya rushwa katika shirikisho la Kandanda Duniani (Fifa), Ijumaa wiki hii shirikisho hilo litamchagua rais mpya kati ya washindani wawili. 

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani Sepp Blatter anawania muhula wa tanu akiwa na umri wa miaka 79.
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani Sepp Blatter anawania muhula wa tanu akiwa na umri wa miaka 79. Reuters/Kim Kyung-Hoon
Matangazo ya kibiashara

Sepp Blatter ambaye anawania muhula wa tanu akiwa na umri wa miaka 79, na mpinzani wake mwanamfalme Prince Ali, mwenye umri wa miaka 39, mmoja wa makamu wake, ambaye pia ametajwa kuwa ni mtu wa mabadiliko, wanawania kinyanga'nyiro hiki.

Je Ali atampiku Blatter ?

Hili ni swali ambalo watu wengi wamekua wakijiuliza. Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya, Michel Platini amemuomba Sepp Blatter kujiuzulu kwenye wadhifa wake bila mafaniko. Sepp Blatter ni rais wa Shirikisho la Soka Duniani tangu mwaka 1998. Blatter anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika kinyanga'nyiro hiki cha uchaguzi. Hata hivyo Blatter huenda akashindwa kutokana na kashfa ya rushwa inayowakabili baadhi ya maafisa wa shirikisho hili la Soka Duniani.

Shirikisho la Soka Duniani lilikumbwa na kizungumkuti baada ya kupigwa na bomu la atomiki kupitia vyombo vya habari kutokana na kesi mbili tofauti za kisheria ziliyofunguliwa na vyombo vya sheria vya Marekani na Uswisi kwa madai ya rushwa kwa kiwango kikubwa, na kukamatwa mjini Zurich kwa maofisa saba wa Shirikisho hilo.

Blatter alijiunga na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) mwaka 1975 kama mkurugenzi wa kiufundi, akawa katibu mkuu (No.2) mwaka 1981, na baadaye kutawazwa kuwa urais. "Ni muhimu kurejesha imani ", Blatter amesema Alhamisi jioni wiki hii wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 65 wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).

Kila shirikisho kwa jumla ya mashirikisho 209 ya Fifa lina kura moja. Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) lina wajumbe 54 lakini lina kura 53 kwa sababu Gibraltar haitambuliwi na Fifa. Gibraltar inampinga Sepp Blatter. Urusi inamuunga mkono Blatter, huku ikibaini kwamba hatua za kisheria ziliyochukuliwa na Marekani ni ujanja ili kuzuia michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2018 isiandaliwi nchini Urusi.

Mareakni iko tayari kumpigia kura mwanamfalme Ali. Kwa sasa soka imeingiliwa na mvutano wa nchini mbili : Marekani na Urusi ambazo uhusiano wao uliingiliwa dosari kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Ukraine.

Afrika ina wajumbe 54 na inaaminika kuwa huenda ikampigia kura Sepp Blatter. Afrika inamchukulia Blatter kama mawanaharakati wa kwanza aliyetetea michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2010 iandaliwe barani Afrika.

Bara la Asia lina wajumbe 46 ikiwemo jordan anakotoka mwanamfalme Ali. Hata hivyo rais wa Shirikisho la Soka barani Asia, Sheikh Salman bin Ebrahim al Khalifa (kutoka Bahrain) ni mfuasi wa Sepp Blatter.

Shirikisho la Soka la Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean (Concacaf), lina wajumbe 35 ambao watapiga kura. Lakini Concacaf imepata pigo kubwa baada ya rais wa Shirikisho hilo kukamatwa. Jeffrey Webb ni mmoja wa maafisa kadhaa wa Fifa waliokamatwa mjini Zurich kufuatia kashfa ya rushwa. Mpaka sasa haijaeleweka iwapo Concacaf itampigia kura Blatter au mwanamfalme Ali. Oceania ina kura 11 na Amerika ya Kusini ina kura 10, kura ambazo hazipewi uzito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.