Pata taarifa kuu
MALI-MAANDAMANO-USALAMA

Mali : maandamano ya kuunga mkono Mkataba wa amani wa Algiers

Maelfu ya waandamanaji walimiminika mitaani jumaane wiki hii katika mji mkuu wa Mali, Bamako kufuatia wito ulitotolewa na vyama vya kiraia na muungano wa vijana ili kuonyesha uungwaji wao mkono kwa Mkataba wa amani uliyotiliwa saini na serikali Mei 15 katika mkuu wa Algeria, Algiers.

REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Watu kutoka tabaka mbalimbali walishiki katika maandamano, ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali, vijana, wanawake kwa wazee wameonekana wakibebelea mabango yaliyoandikwa “ ndio kwa amani nchini Mali ”, huku kwenye mabango mengine kukiandikwa “ Mali haitogawanyika kamwe”, “ amani Kaskazini, Kusini, na katika maeneo yote ya nchi”, au “ waasi mjisalimishe na wekeni silaha chini, tulijnge taifa”

Maandamano hayo yamefanyika kwa utulivu, huku maandamano hayo yakionekana kuipa nguvu serikali. Waandamanaji wamempongeza rais wa nchi hiyo, Ibrahim Boubacar Keïta (IBK), ambaye amechukuliwa na waandamanaji hao kama mtu mwenye busara na uzalendo.

Wakati huo huo waziri mwenye dhamana ya maridhiano, Zahabi Ould Sidi Mohamed, amewahutubia waandamanaji, ambapo amewataka kuwa watulivu na kutumia mazungumzo kama silaha pekee ya kuboresha maridhiano kwa raia wa Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.