Pata taarifa kuu
NIGERIA-INEC-UCHAGUZI-SIASA

Nigeria : chama cha Buhari chashikilia majimbo muhimu

Jumamosi mwishoni mwa juma hili, raia wa Nigeria walipiga kura kwa kuwachagua wakuu wa mikoa 29 pamoja na wajumbe katika baraza la bunge la mikoa kutoka nchi nzima.

kituo cha kupigia kura cha wilaya ya Apapa, Lagos, Aprili 11 mwaka 2015.
kituo cha kupigia kura cha wilaya ya Apapa, Lagos, Aprili 11 mwaka 2015. REUTERS/Akintunde Akinleye
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ulifanyika katika mazingira mazuri, ispokua katika jimbo la Rivers ambapo makabiliano kati ya wafuasi na polisi yalichelewesha uchaguzi.

Tangu jana Jumapili matokeo yamekua yakitangazwa mkoa kwa mkoa, na chama cha APC cha Muhammadu Buhari kinaoneka kupata ushindi mkubwa dhidi ya chama cha PDP cha Goodluck Jonathan.

Mpaka sasa hakuna taarifa zaidi kuhusu matokeo ya uchaguzi katika Jimbo la Rivers kutokana na makabiliano kati ya wafuasi na polisi ambayo yaliendelea hadi Jumapili jioni katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Kulinagana na matokeo ya awali, chama cha PDP cha Goodluck Jonathan kinaonekana kupoteza umaarufu katika ngazi ya kitaifa. Mpaka sasa chama hicho kimekua kikishikilia majimbo 21 kwa jumla ya majimbo 36 dhidi ya 14 ya chama cha APC cha Muhammadu Buhari. Lakini sasa matokeo ya awali yanonyesha kuwa chama cha APC cha Muhammadu Buhari, kilichoshinda uchaguzi wa urais majuma mawili yaliyopita, huenda kikapata uingi wa majimbo 36 ya nchi nzima.

Mpaka jana Jumapili, chama cha APC kilionekana mshindi katika mikoa muhimu, ikiwa ni pamoja na Sokotto, Katsina, Kaduna na lagos.

Matokeo ya jimbo la Adamawa, moja ya majimbo yaliyokumbwa na machafuko ya wanamgambo wa Boko Haramu, hadi jana Jumapili yalikua bado hayajatangazwa, lakini mgombea wa chama cha PDP amebaini kwamba chama cha APC kimeshinda.

Kwa upande wake chama cha PDP, kimeshinda katika majimbo ya Akwa Ibom, katika jimbo lenye mafuta la Niger Delta, kusini mwa Enugu pamoja na kaskazini mwa jimbo la Gombe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.