Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

MONUSCO yatangaza kuanzisha uchunguzi

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zaidi ya raia ishirini waliuawa kwa silaha za jadi kama mapanga na visu karibu na mji wa Beni usiku wa Jumanne na Jumatano wiki hii.

Muili wa mmoja ya watu  waliouawa katika mashambulizi ya kijiji cha Kiddie, kilomita zaidi ya kumi kutoka Beni, Februari 4 mwaka 2015.
Muili wa mmoja ya watu waliouawa katika mashambulizi ya kijiji cha Kiddie, kilomita zaidi ya kumi kutoka Beni, Februari 4 mwaka 2015. AFP PHOTO / KUDRA MALIRO
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya kiraia vinanyooshea kidole waasi wa Uganda ADF-Nalu kuhusika katika mauaji hayo, ingawa kwa sasa, serikali haijathibitisha kuhusika kwa waasi hao katika mauaji hayo.

Baada ya machafuko haya mapya, ujumbe wa Umooja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, umetangaza kuanzisha uchunguzi.

Shambulio hilo limetokea katika kijiji cha Mayangose, kilomita zaidi ya kumi na mji wa Beni. Raia waliohojiwa na RFI wamethibitisha kwamba maefu ya raia katika vitongoji vya Beni, usalama wao uko hatarini.

Mpaka sasa hakuna idadi kamili ya watu waliouawa ambayo imeshatolewa na serikali. Lakini mashirika ya kiraia ambayo yalijielekeza katika eneo la tukio, yamebaini kwamba watu 25 waliuawa kwa mapanga.

Kwa mujibu wa Gilbert Kambale, kiongozi wa vyama vya kiraia katika mji wa Beni, washambuliaji huenda ni waasi wa Uganda wa ADE-Nalu, ambao walihusika katika mauaji ya raia yaliyotokea miezi ya hivi karibuni.

" Tunaamini kuwa ni waasi wa ADF-Nalu waliokua wakiendesha harakati zao mashariki mwa nchi mwaka jana, ambao wakishirikiana na washirika wao waliua watu na wanaendelea kutekeleza kitendo chao hicho kiovu", amesema gilbert Kambale.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.