Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: Monusco yakanusha uvumi wa kushirikiana na waasi wa ADF-Nalu

Tume ya Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo Monusco imeendelea kunyooshewa kidole cha lawama mashariki mwa nchi hiyo, wakati ambapo hali wasiwasi imeendelea kutanda katika baadhi ya maeneo ya ukanda huo.

Monusco yakanusha uvumi unaoipaka matope na kuidhalilisha.
Monusco yakanusha uvumi unaoipaka matope na kuidhalilisha. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja wa Mataifa Monusco imekanusha uvumi wenye lengo la kupotosha raia kwamba tume hiyo imekua ikishirikiana na waasi wa ADF-Nalu kwa kuhatarisha usalama katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kutokana na uvumi huo, Monusco imebaini kwamba huenda shughuli zake zikakwama katika baadhi ya maeneo, kwani raia watakua hawana imani tena na tume hiyo. Monusco imeomba uvumi huo usitishwe.

Tangu majuma kadhaa, raia wa maeneo yaliyo pembezuni mwa Beni wamekua wakiituhumu tume ya Umoja wa Mataifa nchini Congo Monusco kutowajibika kwa kazi yake. Raia hao wamekua wakibaini kwamba helikopta za Monusco zimekua zikiwabeba usiku waasi wa ADF-Nalu.

Inasemekana kuwa Monusco imekua ikiwapelekea chakula na kuwapa msaada wa silaha. Baadhi ya raia wamefikia hadi kusema kwamba Monusco imekua ikiwapa mapanga waasi hao wa Uganda wa ADF-Nalu.

Naibu mkuu wa Monusco, Abdallah Wafy, amebaini kwamba, ADF-Nalu ina wanamgambo wake katika mji wa Beni.

“ Kundi hilo la waasi limewasajili vijana wengi kutoka maeneo ya Beni na vitongoji vyake. Kulingana na takwimu tuliyo nazo, karibu asilimia 40 ya wapiganaji wa ADF-Nalu ni kutoka katika wilaya ya Beni”, amesema Abdallah wafy.

Watu zaidi ya 100 wameuawa hivi karibuni katika mji wa Beni na vitongoji vyake, na kusababisha hali ya usalama kuendelea kudorora katika maeneo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.