Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: vurugu zaibuka Beni

Hali bado ni tete katika mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mamia ya ya wakaazi wa mji wa Beni wameandamana Jumapili Novemba 2 wakisema kughadhibisha na hali ya usalama inayojiri wakati huu katika mji huo, baada ya mauaji ya hivi karibuni ya watu 14.

Mamia ya wakaazi wa Beni wakiandamana dhdi ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Congo Monusco, Oktoba 22 mwaka 2014.
Mamia ya wakaazi wa Beni wakiandamana dhdi ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Congo Monusco, Oktoba 22 mwaka 2014. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Watu 10 waliuawa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Novemba 2 katika pembezuni mwa mji wa Beni. Viongozi wameweka amri ya kutotoka nje ili kujaribio kudhibiti usalama katika eneo hilo.

Nani anaye husika na mauaji hayo? Hilo ni swali ambalo kila mtu amekua akijiuliza katika mji wa Beni. Kwa upande wa viongozi wamebaini kwamba kundi la waasi wa Uganda la ADF-Nalu, ndilo linahusika na mauaji hayo.

Kundi la waasi wa Uganda ADF-Nalu limekua likinyooshewa kidole kuhusika na mauaji katika baadhi ya maeneo ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congoha.

Wakaazi wa mji wa Beni wamekua wakijiuliza pia utaratibu unaotumiwa na wahalifu kwa kutekeleza mauaji hayo, ambapo wahusika wamekua wakiua watu kwa kuwakata kwa mapanga. Baadhi wamesema kwamba huenda waasi hao wa ADF-Nalu wanashirikiana na makundi mengine ya raia wa Congo kwa kutekeleza maovu hayo.

Viongozi wa Congo wamesema kuwa wameanzisha uchunguzi ili kujua waliohusika na mauaji yaliyotokea mwanznoni mwa mwezi Oktoba mwaka 2014 ktiak mji wa Beni na vitongoji vyake. Hata hivo tangu mauaji hayo kutokea hakuna aliye kamatwa ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji katika mji wa Beni, jambo ambalo linaonekana kukwamisha zoezi la uchunguzi.

Hali hiyo ya mdororo wa usalama katika mji wa Beni na vitongoji vyake inapelekea raia kutokua na imani na vikosi vya usalama, na hali hiyo huenda ikasababisha serikali inapoteza imani kwa raia wa maeneo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.