Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: Joseph Kabila awatembelea raia wa Beni

Rais Joseph Kabila Kabange wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo amewasili Jumatano Oktoba 29 mjini Beni mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa Mavivi, wakati wazira yake katika mji wa Beni, Oktoba 29 mwaka 2014.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa Mavivi, wakati wazira yake katika mji wa Beni, Oktoba 29 mwaka 2014. AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Kabila amewasili Beni wiki chache baada ya kufanyika mauaji ya watu zaidi ya themanini, mauaji ambayo inasadikiwa yalitekelezwa na waasi wa Uganda kutoka kundi la ADF-NALU.

Vyanzo vya serikali mjini humo vimesema kuwa rais Kabila anakuja kutoa salaam za rambi rambi kwa familia ziliyofiliwa, lakini pia kutathmini hali ya usalama katika eneo hilo, mara baada ya kufanyika mauaji hayo.

Akizungumza na wakuu wa serikali pamoja na maafisa wa jeshi la nchi hiyo FARDC, Kabila amesema wahusika wa mauaji hayo watachukuliwa hatua kali, huku akibaini kwamba vyombo vya dola vimejipanga kuhakikisha usalama wa wananachi unapewa kipao mbele.

Awali Waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Richard Muyej Mangez, alitangaza kuwa baadhi ya wahusika wa mauaji ya watu zaidi ya 80 katika miji ya Beni na Eringeti wameanza kukamatwa.

Kwa mujibu wa waziri huyo, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haijatupilia mbali pendekezo la kufanyika kwa uchunguzi wa kimataifa lililotolewa na baadhi ya wanasiasa, na kusema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja wahusika wote katika mauaji hayo watakuwa wamekamatwa.

Tamko hilo la waziri wa mambo ya ndani lilitolewa siku moja baada ya kiongozi wa chama cha upinzani cha RCD-KML chenye umaarufu mkubwa katika mji huo wa Beni,Mbusa Nyamwisi, kuelezea kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na waasi wa Uganda wa kundi la ADF-NALU ambao walishirikiana na baadhi ya maofisa wa ngazi ya juu katika jeshi la nchi hiyo ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.