Pata taarifa kuu
LIBYA-IS-Ugaidi-Mauaji-Usalama

Wanajihadi wa IS wajilipua hotelini

Gari ndogo lililokua limetegwa mabomu limelipuka mbele ya moja ya hoteli za kifari katika mji mkuu w Libya, Tripoli. Milio ya risasi imesikika katika shambulio hilo.

Gari lililipuka Jumanne nje ya hoteli katika mji mkuu wa Libya Tripoli.
Gari lililipuka Jumanne nje ya hoteli katika mji mkuu wa Libya Tripoli. Getty Images/Bashar Shglila
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya usalama vimethibisha kwamba wauaji wamejilipua katika hoteli. Tawi la kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam linaloendesha harakati nchini Libya limekiri kuhusika na shambulio hilo.

Watu watatu upande wa vikosi vya usalama wamefariki katika shambulio hilo na wengine watanu wamejeruhiwa.

Inasadikiwa kuwa gari moja au mbili zililipuka mbele ya hoteli Corinthia, Jumanne Januari 27 wakati wa operesheni ya makamando ambayo inaendelea,

Muda mchache baadae watu watatu au wanne walipenya na waliingia ndani ya hoteli, ambayo tangu wakati huo inazingirwa na vikosi vya usalama, kwa mujibu wa shahidi mmoja ambaye amehojiwa kwa simu na RFI.

Kwa mujibu wa msemaji wa operesheni ya usalama katika mmi wa Tripoli, Issam al-Naass, ambaye amehojiwa na shirika la habari la Ufaransa, wauaji “ wametimuliwa na wanazingirwa na vikosi vya usalama katika gorofa ya 21 katika hoteli hiyo”.
Issam al-Naass amebaini kwamba wauaji hao walilipua mikanda yenye vilipuzi waliokua wakivaa.

hoteli Corinthia inatembelewa na wageni wengi, na ni sehemu kuu ya wanadiplomasia na serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.