Pata taarifa kuu
UFARANSA-ALGERIA-Utekaji nyara

Mwili wa mateka wa Ufaransa aliouawa Hervé Gourdel wapatikana

Hervé Gourdel, mtalii wa Ufaransa aliuawa baada ya kutekwa nyara mwezi Septemba mwaka 2014 na wanajihadi.

Hervé Gourdel, mateka wa Ufaransa aliyeuawa mwezi Sepemba mwaka 2014, nchini Algeria.
Hervé Gourdel, mateka wa Ufaransa aliyeuawa mwezi Sepemba mwaka 2014, nchini Algeria. © Facebook/ Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama vilivyonukuliwa na shirika la habari la Ufaransa la AFP, mwili mateka huyo wa Ufaransa ulizikwa katika mlima wa Akbil, kilomita 160 kusini mwa Algiers, ambapo alitekwa nyara na kundi la Jund al-Khilafa.

Muili wake umegunduliwa na jeshi la Algeria, ambalo liilikuwa kufanya operesheni ya kutafuta mwili wake. Nchini Ufaransa, wizara ya mambo ya nje haijathibitisha taarifa hiyo.

Vikosi vya usalama, vikishirikiana na kikosi maalumu cha wanajeshi walikua walitumwa katika eneo lilio karibu na mahali ambapo Hervé Gourdel alitekwa nyara. Mwili wa mateka huyo wa Ufaransa hatimaye umegunduliwa najeshi la Algeria Jumatano Januari 14. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, jaji na mwendesha mashitaka wanasadikiwa kujielekeza eneo la tukio.

Inaonekana kwamba mtu gaidi, aliyekamatwa hivi karibuniambaye alikua miongoni mwa watu waliohusika na kutekwa nyara kwa raia huyo wa Ufaransa, huenda alitoa taarifa ambazo zilipelekea kugunduliwa kwa sehemu alikozikwa mateka huyo. Hervé Gourdel alitekwa nyara mwishoni mwa mwezi Septemba. Video iliyodai mauaji ya Hervé Gourdel ilirushwa hewani Septemba 24 mwaka 2014na kundi la kigaidi la Jund al-Khilafa, "Askari wa Khalifa."

Viongozi wa Algeria waliahidi kushirikiana na vyombo vya sheria vya Ufaransa, lakini taarifa pekee kuhusu uchunguzi zilitolewa wakati wa tangazo la Waziri wa Sheria. Tayeb Louh alitangaza kuwa magaidi wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi, bila kufafanua majina au majukumu ya watu hao katika mauaji ya mtalii huyo wa Ufaransa.

Kwa upande wake, Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa amebaini kwamba wanaendelea kuwasiliana na viongozi wa Algeria. Suala la kuutambua mwili wuliyogunduliwa limepewa kipaumbele. Wizara ya sheria ya Algeria ndio itakayofanya uthibitisho huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.