Pata taarifa kuu
ALGERIA-UFARANSA-Mateka-haki za binadamu-Usalama

Algeria: Muuaji wa Hervé Gourdel atambuliwa

Wiki tatu baada ya Hervé Gourdel, raia wa Ufaransa kutekwa nyara na kuawa, gazeti la El Watan limetangaza Jumamosi Oktoba 11 kwamba mtu aliyehusika na kifo cha mateka huyo ametambuliwa.

Video iliyopelekea kutambuliwa kwa baadhi ya waliomteka nyara  na baadaye kumua Hervé Gourdel.
Video iliyopelekea kutambuliwa kwa baadhi ya waliomteka nyara na baadaye kumua Hervé Gourdel. AFP PHOTO / HO / Jund al-Khilafa via Youtube
Matangazo ya kibiashara

Bachir Kherza, mmoja wa washirika wa karibu wa kiongozi wa kidini wa kundi la wanajeshi wa Khalifa, ametambuliwa na jeshi la Algeria kwamba ndiye alitekeleza mauaji dhidi ya Hervé Gourdel, raia wa Ufaransa aliyetekwa nyara kabla ya kuuawa.

Bachir Kherza ambaye ni mkaazi wa kata ya Bab el-Oued, mjini Algiers nchini Algeria, anatuhumiwa kutekeleza mashambulizi mengi na mauaji ya kigaidi nchini Algeria.

Inaonekana kuwa wanachama mbalimbali wa kundi hilo liliyotekeleza mauaji dhidi ya mateka huyo wa Ufaransa wanatambuliwa kiurahisi, kwa sababu vyombo vya usalama vilifaulu kutambua watu thelathini kufuatia video iliyorushwa kupitia mtandao wa kundi hilo. Kama Abu Abdullah al-Othman Assimi, anayeshukiwa kuandaa operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na kundi la wanajeshi wa Khalifa au Abdelmalek Gouri, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kundi hilo.

Watu hao ni kutoka vitongoji maarufu mjini Algiers au katika eneo la Boumerdès mashariki ya huo wa Algiers. Baadhi yao walikua wanachama wa kundi la Salafist linaloendesha karakati za kuhubiri na kupambana (GSPC) na baadaye walijiunga na kundi la Aqmi lenye mafungamano na Al-Qaeda. Haijulikani iwapo watu hao walitambuliwa na jeshi baada ya kupeleleza waliko

Ijumaa wiki hii, jeshi la Algeria limefahamisha kwmba limewaua magaidi watatu wakati wa operesheni ya kijeshi katika jimbo la Kabylie, bila hata hivo kutoa taarifa zaidi iwapo watu hao walikua na uhusiano na kundi la wanajashi wa Khalifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.