Pata taarifa kuu
UGANDA-LRA-MAREKANI-CAR-USALAMA-SHERIA

Mmoja wa viongozi wa juu wa LRA ajisalimisha

Mtu anayedai kuwa mmoja wa makamanda wa juu wa kundi la waasi la LRA kutoka nchini Uganda, anazuiliwa na wanajeshi wa Marekani.

Waasi wa LRA mwezi Septemba mwaka 2006 katika mpaka kati ya Sudan na DRC.
Waasi wa LRA mwezi Septemba mwaka 2006 katika mpaka kati ya Sudan na DRC. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Mtu huyo anayejiita Dominic Ongwen alijisalimisha kwa wanajeshi wa Marekani, kwa mujibu wa ripoti za Wizara ya ulinzi ya Marekani.

Ongwen anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Joseph Kony akiwa Sudani Kusini mwaka 2008.
Joseph Kony akiwa Sudani Kusini mwaka 2008. REUTERS/Africa24 Media

Ongwen amekuwa akielezwa kuwa naibu wa kiongozi wa LRA, Joseph Kony, anayetafutwa na wanajeshi wa Marekani na wale wa Umoja wa Afrika.

Serikali ya Marekani imeendelea kuthibitisha taarifa hiyo ya kujisalimisha kwa mmoja wa makamanda wa juu wa kundi la waasi wa Uganda la Lords Resistance Army LRA.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Jane Psaki, Dominic Ongwen anayedai kuwa ni mmoja wa watu wa karibu wa kiongozi wa kundi la LRA linaloongozwa na Joseph Kony, amejisalimisha kwa wanajeshi wa Marekani.

 

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa iwapo itathibitika kuwa mtuhumiwa huyu ni mtu wa karibu wa Kony, itakuwa pigo kwa kundi hili ambalo linaendesha harakati zake kwenye misitu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.