Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-BOTSWANA-EFF-MALEMA-DIPLOMASIA-USALAMA

Viongozi 6 wa EFF wapigwa marufuku kuingia Botswana

Serikali ya Botswana imepiga marufuku viongozi 6 wa chama cha EFF kinachoongozwa na Julius Malema raia wa Afrika Kusini kuingia katika ardhi yake. Botswana imekua ikiwatuhumu viongozi hao kuwa  na lengo la kuhatarisha usalama wake.

Julius Malema, kiongozi wa zamani wa kundi la vijana wa chama tawala Afrika Kusini (ANCYL), akiwa pia kiongozi wa chama kipya cha upinzani EFF.
Julius Malema, kiongozi wa zamani wa kundi la vijana wa chama tawala Afrika Kusini (ANCYL), akiwa pia kiongozi wa chama kipya cha upinzani EFF. REUTERS/Peter Andrews
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa zamani wa vijana wa chama tawala Afrika Kusini (ANCYL), ambaye kwa sasa ni kiongozi wa chama kipya cha upinzani cha EFF, Julius Malema na viongozi wengine 5 wa chama hicho wamepigwa marufuku kuingia Botswana.

Hivi karibuni kiongozi wa chama cha EFF, Julius Malema alibaini kwamba Botswana imekua ikiruhusu mataifa ya kigeni kuweka kambi za kijeshi katika aridhi yake.

Malema amekua akiikosoa serikali ya Botswana na kuwataka raia wa Botswana kushirikiana na vyama vya upinzani pamoja na chama chake kwa kupinga sera za chama tawala nchini Botswana pamoja na mpango wa serikali ya nchi hiyo wa kuendelea kuruhusu mataifa ya kigeni kuweka kambi za kijeshi katika aridhi ya Botswana.

Mwezi Julai mwaka 2013, serikali ya Botswana ilimlazimisha Julius Malema kulipia visa ili aweze kuruhusiwa kuingia nchini Botswana.

Hatua hiyo iliyochapishwa katika gazeti la serikali iliwalenga pia raia kutoka Uingereza, Gordon Bennett, Joseph Bennett pamoja na Kate Elizabeth Holberton.

Raia wa Afrika Kusini na Uingereza hawahitaji kulipia visa kwa kuingia nchini Botswana.

Wakati huo Malema aliituhumu serikali ya Ian Khama kwa kuwakandamiza raia wake, huku akithibitisha kwamba ni serikali hiyo “mtumwa wa nchi za magharibi”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.