Pata taarifa kuu
TUNISIA-Uchaguzi-Siasa

Tunisia: uchaguzi wa wabunge wafanyika

Chama kikuu cha nchini tunisia kimedhihirisha kuwa na imani katika zoezi la uhesabuji kura siku moja baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge.

wanajeshi wa kikosi cha usalama wa taifa wakiimarisha ulinzi katika katika kituo kimoja cha kupigia kura mjni Tunis.
wanajeshi wa kikosi cha usalama wa taifa wakiimarisha ulinzi katika katika kituo kimoja cha kupigia kura mjni Tunis. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Raia nchini Tunisia wamewachagua wabunge 217. Askari polisi 80,000 walikua wametumwa nchi nzima kuimarisha ulinzi katika vituo vya kupigia kura.

Uchaguzi huo wa wabunge unachukuliwa kuwa ni wa kihistoria, ambao ulilenga kuimarisha demokrasia nchini humo tangu mapinduzi ya kiarabu kutokea mwaka 2011.

Uchaguzi huo wa wabunge ulifanyika Jumapili Oktoba 26, chini ya ulinzi mkali wa kijeshi kwa tahadhari ya mashambulizi ya wapigania wa kijihadi.

Taifa hilo la Afrika Kaskazini limekuwa na dalili za matumaini likilinganishwa na mataifa ya Libya na Misri ambayo yalikumbwa na ghasia na tawala kupinduliwa.

Hata hivyo mageuzi taifa hilo la Tunisia yamekuwa yakijaribiwa mara kadhaa kwa mashambulizi ya wanamgambo na ghasia za ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.