Pata taarifa kuu
NIGERIA-ONYO

Obasanjo: Lazima wasaliti watafutwe na kufunguliwa mashtaka kwa kushirikiana na magaidi

Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo amesema kuwa ni lazima Serikali yake na mataifa ya Afrika magharibi yashirikiane kuwasaka viongozi wa Serikali na wale wa vyombo vya usalama ambao wamekuwa wakila njama na kundi la Boko Haram nchini Nigeria kutekeleza uasi unaoshuhudiwa kaskazini mwa nchi hiyo na kwenye baadhi ya mataifa ya ukanda wao. 

Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo
Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza akiwa mjini Dakar ambako mkutano wa kupinga matumizi ya dawa za kuelvya unafanyika nchini Senegal, rais huyu msaatafu wa Nigeria ambaye ni mwenyekiti wa tume ya kupambana na dawa za kulevya kwa nchi za magharibi mwa Afrika, anataka kuona maofisa wa Serikali wanaopewa fedha na kundi hilo kwa lengo la kuvujisha taarifa wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Obasanjo ameongeza kuwa licha ya migogoro ya ndani ambayo inachangiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, tatizo la matumizi ya dawa za kuelvya kwenye ukanda huo pia ni changamoto nyingine.

Kwa upande wake aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan ambaye anahudhuria mkutano huo, yeye anasisitiza umuhimu wa mataifa ya magharibi mwa afrika kuunganisha nguvu kukabiliana na wimni la kuenea kwa dawa za kulevya.

Tume ya kupambana na dawa za kuelvya kwa nchi za Afrika Magharibi imesema kuwa kutokana na sera zilizopo, zimeruhusu kuwepo kwa ongezeko la rushwa ambapo nchi hizo zimekuwa zikipoteza kiasi cha dola bilioni 1.25 kwa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.