Pata taarifa kuu
NIGERIA-Usalama

Nigeria: Obasanjo ajitolea kuwa msuluhishi kati ya serikali na Boko Haram

Serikali ya Nigeria inaendela kupata vishawishi ili kuwapata wasichana waliyotekwa nyara na kundi la wanamgambo wa kislamu la Boko Haram katikati ya mwezi wa Aprili mwaka huu wa 2014.

Rais wa zamani wa Nigeria Nigeria Olusegun Obasanjo akisema yuko tayari kusuluhisha serikali na kundi la Boko Haram kwa la kuwapata wasichana waliotekwa nyara.
Rais wa zamani wa Nigeria Nigeria Olusegun Obasanjo akisema yuko tayari kusuluhisha serikali na kundi la Boko Haram kwa la kuwapata wasichana waliotekwa nyara. AFP / Seyllou
Matangazo ya kibiashara

Mike Okiro, mkuu wa pilisi nchini Nigeria.
Mike Okiro, mkuu wa pilisi nchini Nigeria. (Photo : AFP)

Mapema jumanne wiki hii, jeshi la Nigeria lilithibitisha kwamba, baada ya kufanya uchunguzi wake linafahamu sehemu waliko wasichana hao, lakini Marekani imefahamisha kwamba haijapata uthibitisho kutoka serikali ya Nigeria wala haina ushahidi wowote wa kufahamu sehemu waliko wasichana hao.

Hata hivo kuna habari zinazofahamisha kwamba kumekua na jaribio la kuanzisha mazungumzo na kundi la Boko Haram bia mafaanikio.

Wakati huo huo rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ameanzisha mchakato wa mazungumzo na upatanishi baina serikali na kundi la kigaidi la Boko Haram linaloendelea kuwashikilia wasichana wanafunzi zaidi ya 200 sehemu kusikojulikana.

Wakati hayo yakijiri, Jeshi la Cameroon limerundika askari upande wa mipaka ya nchi hiyo karibu na mkoa wa kaskazini ambako matukio ya ugaidi yamekithiri na hatua ya kukabiliana na tishio la kundi hilo la kiislamu la Nigeria.

Kati ya askari 1,000 hadi 3,000 tayari wamejihami kivita dhidi ya Boko Haram ikiwa ni moja ya hatua ya utekelezwaji wa makubaliano baina ya serikali hizo mbili, kama anavyobainisha Issa Tchiroma Bakary, Waziri wa Habari wa Cameroon na msemaji wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.