Pata taarifa kuu
NIGERIA-Usalama

Nigeria: mashambulizi mawili tofauti katika mji wa Jos yasababisha vifo vya watu wengi

Mashambulizi mawili tofauti yameutikisa mji wa Jos nchini Nigeria jana alaasiri, kulingana na taarifa iliyotolewa na idara ya kitaifa ya kukabiliana na majanga, watu 118 wameuawa katika mashambulizi yaliyolenga soko ambayo inatembelewa na watu wengi katika mji huo wa Jos.

Mabaki ya gari iliyotumiwa katika shambulizi liliyotokea katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria, May 19 mwaka 2014.
Mabaki ya gari iliyotumiwa katika shambulizi liliyotokea katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria, May 19 mwaka 2014. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Polisi kwa upande wake imebaini kwamba watu 46 ndio wameuawa katika milipuko hio. Mji wa Jos unapatikana katika jimbo la Plateau kati ya ya eneo la kusini lenye wakristo wengi na kaskazini lenye waislamu wengi.

Milipuko hio ya mabomu ilipishana kwa muda wa dakika thelathini. Mashahidi wamesema wameona miili ya watu na majeruhi ambao baadhi ya viongo vikiokotwa wakiondolewa kwenye eneo la tukio.

Washambuliaji walitumia gari ndogo, na bomu lingine lilitegwa ndani ya basi ambayo ilikua iliegeshwa kwenye barabara inayo elekea hospitali ambako walikua wakisafirishwa wahanga wa mashambulizi hayo karibu na soko kulikotokea shambulio la kwanza.

Vyombo vya habari nchini Nigeria vimebaini kwamba waokozi wengi wamehariki katika mashambulizi hayo, lakini polisi imefahamisha kwamba wengi mwa wahanga ni wanawake.

Nigeria inakumbwa na mfululizo wa mashambulizi.
Nigeria inakumbwa na mfululizo wa mashambulizi. REUTERS/Stringer

Wanawake wengi wanauzia bidhaa zao wapita njia katika baadhi ya mitaa ya Jos, huku kukiwa na msongamano wa mabasi na treni kwenye barabara mbalimbali za mitaa hio.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan akilani mashambulizi yaliyoutikisa mji wa Jos katika jimbo la Plateau.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan akilani mashambulizi yaliyoutikisa mji wa Jos katika jimbo la Plateau. REUTERS/Afolabi Sotunde

Haraka sana rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amelaani mashambulizo hayo na kuwataka waliyotekeleza kama watu wasiopenda uhuru wa binadamu. Hakuna kundi liliojitokeza kudai kutekeleza mashambulizi haya, lakini kundi la kigaidi la Boko Haram linashukiwa tayari limenyooshewa kidole.

Mji wa Jos ulikua haujashuhudia tukio la kigaidi kwa kipindi cha miaka minne baada ya mfululizo wa mashambulizi yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa kislamu la Boko Haram katika mitaa inyokaliwa na watu kutoka jamii ya wakristo mwezi desemba mwaka 2010.

Mashambulizi haya huenda yakakuza chuki na kusababisha machafuko yenye misingi ya kidini.

Tayari viongozi wa dini mbalimbali katika mji wa Jos wametolea wito raia wa kuvumiliana na kutojihusisha na ulipizaji kisase.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.