Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Rais wa Nigeria apuuza matakwa ya Boko Haram

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amekataa pendekezo la kundi la kigaidi la boko Haram kuwaachilia wanamgambo wake wanaozuiliwa ili kundi hilo liwaachilie huru wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara mwezi mmoja uliopita.

Rais wa Nigeria, Goofdluck Jonathan,akikataa matwa ya kundi la Boko Haram ya kubadilishana wanamgambo wa kungi hilo na wasichana waliyotekwa nyara.
Rais wa Nigeria, Goofdluck Jonathan,akikataa matwa ya kundi la Boko Haram ya kubadilishana wanamgambo wa kungi hilo na wasichana waliyotekwa nyara. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Uingereza anayehusika na maswala ya Afrika Mark Simmonds amewaambia waandishi wa habari jijini Abuja kuwa walizungumzia suala hilo na rais Jonathan akakataa kushauriana na kundi hilo kuhusu kuachiliwa kwa wafungwa hao.
Hata hivyo, waziri huyo wa Uingereza amesisitiza kuwa serikali ya Nigeria iko tayari kuzungumza na kundi hilo ili kuachiliwa huru wasichana hao na kutokomeza vitendo hivyo vya ugaidi nchini humo.

Aboubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram, katika mkanda wa video uliyorushwa hewani mei 12 mwaka 2014.
Aboubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram, katika mkanda wa video uliyorushwa hewani mei 12 mwaka 2014. AFP PHOTO / BOKO HARAM

Kiongozi wa kundi la Boko Haram, abubakar Shekau, alipendekeza fikra hio ya kubadilichana wasichana waliyotekwa nyara na wanamgambo wa kundi lake wanaozuiliwa katika mkanda wa video uliyorushwa hewani jumatatu, huku ukiwaonyesha wasichana hao waliyotekwa nyara katika shule la Chibok, linalopatikana katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mapema juzi jumanne, waziri wa mambo ya ndani Abba Morro alipinga pendekezo hilo, huku akikatalia kundi la Boko Haram kutoa mashari, iwapo itataka mazungumzo na serikali.

Wakati huo huo juzi jumanne waziri wa masuala maalum, Taminu Turaki, alisema serikali ya Nigeria iko tayari kuketi pamoja na kundi la Boko Haram ili mradi tu wasichana waliyotekwa nyara waachiliwe.

Mkanda wa video uliyorekodiwa na kundi la Boko Haram ukionyesha wasichana waliyotekwa nyara na wanamgambo wa kundi hilo nchini Nigeria.
Mkanda wa video uliyorekodiwa na kundi la Boko Haram ukionyesha wasichana waliyotekwa nyara na wanamgambo wa kundi hilo nchini Nigeria. AFP

Kwa sasa Marekani inaongoza operesheni maalum wakitumia ndege maalum kuwatafuta wasichana hao ambao hawajulikani walipo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.