Pata taarifa kuu
JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO-MONUSCO-Usalama

Monusco yajiandaa kuondoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linajiandaa kuondoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuwa nchini humo kwa zaidi ya miaka kumi. 

Martin Kobler, mkuu wa vikosi vya Umoja wa Matiafa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Martin Kobler, mkuu wa vikosi vya Umoja wa Matiafa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. RFI
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kinshasa, mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Martin Kobbler, amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya azimio namba 2147 lililopitishwa hivi karibuni na Baraza la Usalama inayobaini kwamba wamo katika mchakato wa kuandaa namna ya kuondoka kwa vikosi Vya kulinda amani vya MONUSCO Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kobler ameongeza kuwa vikosi hivyo vya MONUSCO ambavyo idadi yao imefikia 20.000 vitatakiwa kuondoka nchini humo mara baada ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kuwasilisha ripoti kwa Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwaka huu inayozungumzia mpango wa vikosi hivyo kuanza kuondoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Baraza la Usalama limepitisha azimio hilo kuongeza muda wa mwaka moja kwa ajili ya vokosi hivyo kuendelea kupambana na makundi ya waasi.

Vikosi hivyo ambavyo vilianza kujulikana kwa jina la MONUC, vilianzishwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwaka 1999, na idadi ya vikosi hivyo iliendelea kuongezeka hadi kufikia 20.000.

Vikosi hivyo vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vilikua vikinyooshewa kidole cha lawama na raia wa mashariki mwa taifa hilo kwamba haviwajibiki ipasavyo katika majukumu yao ya kulinda usalama wa raia.

Lakini matumaini kwa raia na pongezi kwa vikosi hivyo vilikuja baada ya jeshi la Congo kuanzisha operesheni kwa ushirikiano na kikosi maalumu cha Monusco iliyo ktokomeza kundi la waasi la M23, novemba mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.