Pata taarifa kuu
JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO-Usalama

Mji wa Lukweti mashariki mwa DRC washikiliwa kwa sasa na majeshi ya serikali

Majeshi ya serikali ya DRCongo FARDC yamerejesha kwenye himaya yake mji wa Lukweti ulio mashariki mwa nchi hiyo ambao ulikuwa unakaliwa na waaasi tangu kipindi cha miaka sita iliopita. Msemaji wa vikosi vya serikali katika mkoa wa kaskazini mwa Kivu Kanali Olivier Hamuli amethibitisha taarifa hii na kusema kwamba wamemfukuza mbabe wa kivita Janvier Karairi na watu wake katika mji huo.

Kikosi cha wanajeshi wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mashariki mwa nchi
Kikosi cha wanajeshi wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mashariki mwa nchi RFI
Matangazo ya kibiashara

Lukweti inapatikana katika tarafa ya masisi kwenye umbaliw akilometa 80 kaskazini magharibi mwa mji wa Goma, mji mkuu wa Mkoa wa Kivu ya Kaskazini. Olivier Hamuli amesema kulikuw ana mapigano ambayo yalisabahisha mbabe huyo wa kivita Janvier Karairi wa kundi la APCLS kutoroka na kundi lake.

Jeshi la FARDCA limekuwa katika mapambano tangu majuma kadhaa na waasi wa kundi hilo la APCLS ambapo March 9 jeshi la Congo lilipata msaada kutoka kwa vikosi vya Monusco ambapo helikopta ya kijeshi ilishambulia vituo vilivyokuwa vinakaliwa na wapiganaji wa kundi hilo la waasi.

Kundi hilo la APCLS ambalo linasadikiwa kuwa na wapiganaji 500 liliundwa tangu mwanzoni mwa mwaka 2008 ambapo liliundwa kwa kiasi kikubwa na wapiganaji kutoka kabila la wa Wahunde waliokuwa wanapinga mizozo ya ardhi dhidi ya watutsi kaskazini mwa Mkoa wa Kivu ambao wanasema sio raia wa DRCongo.

Kwa mujibu wa wataalamu wa Mkoa wa Kivu ya kaskazini wawakilishi wa kundi la APCLS na wa makundi mengine kama vile Raia Mutomboki, na kundi la wapiganaji wanaoongozwa na Ntbo Taberi Sheka wamekutana siku ya Ijumaa iliopita kwa ajili ya kuanzisha muungano wa kuwazuia raia wa kabila la watutsi waliokimbilia nchini Rwanda kutorejea nchini DRCongo.

Baada ya ushindi dhidi ya waasi wa kitutsi wa kundi la M23 novemba mwaka jana, serikali ya Kinshasa imeanzisha harakati za kuwarejesha nyimbani wakimbizi waliokimbilia nchini Rwanda tangu mwaka 1990.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.