Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Morgan Tsvangirai agadhabishwa na tarehe ya Uchaguzi Mkuu nchini Zimbabwe

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai, amepinga mpango wa rais Robert Mugabe kuwa uchaguzi Mkuu ufanyike tarehe 31 mwezi ujao kwa kile anachosema kuwa rais huyo anakiuka katiba ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Tsvangirai kwa gadhabu ameongeza kuwa Mugabe anasababisha malumbano ya kisiasa nchini humo na badala yake anataka uchaguzi huo kufanyika tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu suala ambalo anasisitiza kuwa atafika Mahakamani  kutafuta uungwaji mkono.

Aidha, Tsvangirai amesema kuwa Mugabe amekuwa akikiuka makubaliano ya uundwaji wa serikali ya muungano iliyoundwa mwaka 2008 baada ya machafuko ya baada ya uchaguzi Mkuu ya inayowataka kufanya maamuzi ya serikali  pamoja baada ya mashauriano.

Waziri Mkuu huyo amesisitiza kuwa hawezi kukubali tarehe hiyo ya uchaguzi kwa sababu hakushauriwa na rais Mugabe kama inavyohitajika kisheria inayounda serikali ya muungano inayompa mamlaka sawa na Mugabe.

Kiongozi huyo wa chama cha MDC amesisitiza kuwa uchaguzi huru na haki hauwezi kufanyika nchini humo ikiwa shirika la habari la serikali na idara za usalama hazitafanyiwa mabadiliko muhimu.

Mapema siku ya Alhamisi, rais Mugabe kwa upande wake alisisitiza kuwa uchaguzi huo utafanywa kama ilivyopangwa tarehe 31 mwezi ujao na hauwezi kuahirishwa.

Mugabe mwenye umri wa miaka 89 ameongoza nchi hiyo kwa miaka 33, anatarajiwa kuwania tena urais wa mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.