Pata taarifa kuu
MAREKANI-UGANDA

Marekani yatangaza zawadi ya Dola Milioni 5 kwa atayakayefanikisha kukamatwa kwa Kiongozi wa LRA Joseph Kony

Serikali ya Marekani imetangaza zawadi ya dola milioni tano kwa yoyote ambaye atafanikisha kukamatwa kwa Kiongozi wa Kundi la Waasi la Lord's Resistance Army LRA Joseph Kony anayesakwa kwa udi na uvumba.

Kiongozi wa Kundi la Waasi la LRA Joseph Kony ambaye Serikali ya Marekani imetenga dola milioni tano kufanikisha kukamatwa kwake
Kiongozi wa Kundi la Waasi la LRA Joseph Kony ambaye Serikali ya Marekani imetenga dola milioni tano kufanikisha kukamatwa kwake
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Marekani imeamua kutangaza zawadi hiyo kutokana na operesheni za kumsaka Kony kuonekana kugongwa mwamba huku Uganda wakitangaza kusitisha msako waliokuwa wanaufaya kwa muda.

Kony anasakwa kutokana na kutenda makosa ya uhalifu wa kivita ikiwemo kuajiri watoto wadogo kwenye jeshi lake pamoja na Kundi lake kutekeleza vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake.

Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani imetangaza zawadi hiyo kama sehemu ya kuongeza chachu opesherni ya kuhakikisha Kony anapatikana huku pia Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC ikimhitaji kujibu mashtaka yanayomkabili.

Miongoni mwa watu wa karibu wa Kony ambao nao wanasakwa ni pamoja na Okot Odhiambo na Dominic Ongwen ambao wote wanatajwa kuwa sehemu ya mpango wa kutekelezwa kwa makosa ha uhalifu wa kivita.

Kony ameingia kwenye orodha ya Vinara wa Uasi wanosaka kwa udi na uvumba na Marekani wakiwa wanafanya shughuli zao Barani Afrika akiwemo Sylvestre Mudacumura anayetoka Kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda FDLR.

Kiongozi huyo wa Kundi la Waasi la LRA amekuwa kitajwa kutekeleza mashambulizi katika nchi za Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan huku sehemu ambayo anajificha ni kwenye misitu iliyopo Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Serikali ya Kampala imekuwa ikimsaka Kony bila ya mafanikio na hata ikafikia hatua ya kupeleka jeshi lake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ajili ya zoezi hilo lakini hawajafua dafu.

Serikali ya Uganda imetangaza kusitisha kwa muda msako wa Kony kutokana na kutokea kwa mapinduzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na kusababisha serikali ya Rais Francois Bozize kuangushwa na Kiongozi wa Muungano wa Seleka Michel Djotodia kuchukua madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.