Pata taarifa kuu
ANGOLA

Waangola wapiga kura katika uchaguzi unaokisiwa kuwa rais wa sasa Jose Eduardo dos Santos atashinda .

Wananchi wa Angola wamepiga kura leo Ijumaa kumchagua rais katika uchaguzi wa tatu wa nchi hiyo tangu uhuru mwaka 1975, huku Rais Jose Eduardo dos Santos akitarajiwa kuongeza muda wake wa kuiongoza nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta licha ya upinzani kuongezeka. 

euronews.com
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Luanda ambao kwa kawaida hufurika watu, umekuwa katika hali ya ukimya isivyo kawaida kufuatia Ijumaa ya leo kutangazwa kuwa siku ya mapumziko ili kuruhusu raia wapatao milioni 9.7 waliojiandikisha kupiga kura kushiriki zoezi hilo katika vituo zaidi ya elfu kumi vilivyoandaliwa.

Zoezi la Kupiga kura limeendelea polepole huku kukiwa na vikwazo vichache , jambo linalodhihirisha maboresho makubwa kutoka kufanyika kwa uchaguzi uliopita mwaka 2008 ambapo zoezi hilo liliongezwa siku kutokana na machafuko katika vituo vya kupigia kura.

Chama cha upinzani cha Unita kimeelezea wasiwasi wake kuwa uchaguzi huo huenda usiwe huru na wa haki.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.