Pata taarifa kuu
Sudani

Omar Al Bashir akubali mazungumzo na Sudan Kusini, Mbeki aelekea Juba

Mpatanishi wa umoja wa Afrika kwenye mgogoro wa Sudani na Sudani Kusini Thabo Mbeki anaelekea Sudani Kusini kuendelea na jitihada za kushinikiza mataifa hayo mawili kurejea katika meza ya mazungumzo.

AFP/ Kambou Sia
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kumalizika kwa siku mbili za mazungumzo na maofisa wa serikali ya Sudani Khartoum siku ya Jumamosi rais Mbeki anaelekea Juba kuendeleza jitihada hizo za ushawishi wa mazungumzo.

Akiwa Khartoum Mbeki amesema kuwa rais Omar al Bashir amekiri kuwa ipo haja ya nchi hizo kurejea katika mazungumzo ya kutafuta amani na kwamba nchi yake ina dhamira ya dhati katika mikataba ya amani iliyotia saini.

Sudan na Sudan kusini hazikutekeleza matakwa ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuzitaka kuanza mazungumzo Jumatano iliyopita, lakini Mbeki na wanadiplomasia wengine wameendelea kujaribu kuzirejesha nchi hizo katika mazungumzo.

Sudani Kusini kwa upande wake imesema iko tayari kurudi katika meza ya mazungumzo lakini inaituhumu Sudani kwa kugoma kufanya hivyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.