Pata taarifa kuu
SOMALIA-SUDAN-KENYA-MAREKANI

Umoja wa Mataifa UN wahitaji msaada wa dola bilioni 7.7 kusaidia nchi za Pembe ya Afrika

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kupitia Tume ya Misaada ya Umoja huo imetoa wito kwa mataifa duniani kuchanga jumla ya dola bilioni saba nukta saba ili kuzisaidia nchi za Pembe ya Afrika zinazokabiliwa na ukame uliochangia uwepo wa njaa.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya Misaada ya Umoja wa Mataifa UN imezigeukiwa nchi kumi na sita zenye nguvu kiuchumi kuweza kufanikisha kusaidia mataifa ya Pembe ya Afrika kuweza kupata chakula cha kutosha kwa ajili ya wananchi wao.

Hiki ni kiwango kukibwa zaidi cha fedha ambacho kimeombwa na Tume hiyo ya Misaada kuweza kuzisaidia nchi za Somalia, Sudan na Kenya kuweza kumaliza tatizo la ukame na njaa linaloshuhudiwa kwa sasa.

Tume ya Misaada ya Umoja wa Mataifa UN tayari imeshatenga jumla ya dola bilioni moja nukta tano kwa ajili ya Mfuko wa kuisaidia Somalia ambayo watu wake laki mbili na elfu hamsini wapo hatarini kupoteza maisha.

Mkuu wa Tume ya Misaada Valerie Amos amesema mataifa hayo yanawajibika ifikapo mwanzoni mwa mwaka elfu mbili na kumi na mbili wame wameweza kupata nusu ya fedha zote ambazo zinahitajika.

Kenya peke yake inahitaji jumla ya dola milioni mia saba na sitini na nne ifikapo mwaka elfu mbili na kumi na mbili ili kuweza kukabiliana na ukosefu wa chakula unaokabili eneo la Pembe ya Afrika.

Wananchi milioni kumi wa Somalia nao wanahitaji msaada wa haraka ikiwemo wa chakula na ukame unaoizingira nchi hiyo kwa muda mrefu sasa huku suluhu yake ikishindwa kupatikana kwa wakati.

Nchi za Sudan na Sudan Kusini zimeendelea kujikuta katika wakati mgumu ambao umekuwa ukichangiwa na uwepo wa vita katika eneo la mpaka wa mataifa hayo mawili na kusababisha uwepo wa ukame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.