Pata taarifa kuu
TANZANIA

Tanzania yaadhimisha miaka 12 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa baba wa taifa Julius k.Nyerere

Wananchi wa Tanzania leo wanafanya kumbukizi ya miaka kumi na miwili tangu kutokea kwa kifo cha Muasisi wa Taifa hilo na Mwanaharakati wa Mapinduzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwl. Julius K. Nyerere
Mwl. Julius K. Nyerere Tanzania.org
Matangazo ya kibiashara

Kumbukumbu hii inafanyika huku mwenendo wa siasa za Tanzania zikikosolewa vikali kutokana na wengi kuamini kuwa falsafa ambayo aliijenga Mwalimu Nyerere imepewa kisogo na wanasiasa wa taifa hilo.

Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania wamesema kuwa viongozi wengi wameshindwa kumuenzi kiongozi huyo kwa maneno na vitendo jambo linalochangia kuwepo kwa mpasuko wa kisiasa na ubadhirifu uliokithiri ambao unachangia kuliletea taifa hasara na kurudisha nyuma maendeleo.

Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa mkoani Mara katika kijiji cha Butiama ambapo mamia ya watanzania wakiongozwa na makamu wa raisi Dokta Gharib Bilali sambamba na viongozi wa serikali na madhehebu ya dini wamehudhuria maadhimisho hayo ya kumi na mbili tangu kutokea kwa kifo cha kiongozi huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.