Pata taarifa kuu
Swaziland

Mfalme wa Swaziland aomba IMF na benki ya dunia kuikoa Swaziland

Mfalme wa Swaziland, mswati wa 3 ameomba shirika la fedha duniani na benki ya Dunia kuiokoa Swaziland kama ilivyofanya kwa ugiriki na Portugal.

Mfalme Muswati 3 wa Swaziland
Mfalme Muswati 3 wa Swaziland
Matangazo ya kibiashara

Mswati amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa mazungumzo juu ya namna ya kuondokana na mgogoro wa kiuchumi nchini humo.

Vyama vya wafanyakazi walioandaa maandamano dhidi ya serikali wiki iliyopita, wamesusia mkutano huo huku polisi ikizuia maandamano yaliyokuwa yakifanywa na makundi ya dini na ya asasi za kiraia makundi hayo yanamshutumu Mswati kwa kulifilisi taifa kwa mtindo wake wa maisha ikiwemo wake zake kumi na watatu kila mmoja na kasri yake.

IMF imekataa kuipa mkopo Swaziland mpaka serikali ya nchi hiyo itakapochukua hatua kubana matumizi, ikiwemo kupunguza mishahara, na kupunguza bajeti ya safari na kutilia maanani maswala ya afya na elimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.